Je, kuku aina ya broiler hawafugiki kienyeji?

Je, kuku aina ya broiler hawafugiki kienyeji?

Simeone

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
905
Reaction score
1,002
Hivi broiler nikiwafuga kienyeji, yaani wajitafutie chakula kwani kuna shida gani?
 
Binafsi huwa napenda kuwafuga kienyeji but wakiwa Wakubwa ......huwa wanakuwa vzr
 
Umeshawahi kuwafuatilia hata kwa masaa mawili tu ujue wanakula chakula na maji kwa kiasi gani?Hicho chakula tu lazima kiende pamoja na mchanganyiko wa dawa mbalimbali pembeni maji ya kunywa mengi.Umejiandaaje kuwakabili pakashume,vicheche na mijibwa mijizi watakaowanyemelea wawatafune?Kama unataka wawe ma-models,sawa!
 
Wanafugika tu. Ila akisha pandwa anadata kabisa na dyudyu, anaweza kuhama kwako akahamia nyumbani kwa kina jogoo
Je unatumia kiatamishi ili kuangua mayai?
 
Umeshawahi kuwafuatilia hata kwa masaa mawili tu ujue wanakula chakula na maji kwa kiasi gani?Hicho chakula tu lazima kiende pamoja na mchanganyiko wa dawa mbalimbali pembeni maji ya kunywa mengi.Umejiandaaje kuwakabili pakashume,vicheche na mijibwa mijizi watakaowanyemelea wawatafune?Kama unataka wawe ma-models,sawa!
Sijawahi mkuu! je nikimpa chakula bila dawa kuna tatizo?
 
Wana malezi na ukuaji tofauti na wetu wa asili.Usidanganyike kuwabwaga tu na kuendelea na mambo yako,utakula hasara.
Mimi lengo langu ni kukwepa kununua chakula dukani maana nasikia zina gharama sana ila kama ni chanjo nawapatia

chakula nataka niwe nawapa pumba za mahindi, je hapo nitakuwa nimepunguza hasara ambayo ningeweza kuipata?
 
Fb kuna mtu kakujibu vizuri.Rudi umsome.
 
Nakumbuka kuna kipindi nilikuwa mkoa,Mzee akanunua mmoja alikuwa ni dume,mwanzo alipata tabu kuyaishi maisha ya kujitafutia, ila mwisho wa siku akayazoea akajanjaruka na mwisho wa siku alitusaidia sana kutupatia mbegu zake tulipata machotara majike na madume karibia uzao wake wote,
 
Back
Top Bottom