Je, kuna bima ya kilimo? Kama hakuna. Nini tija ya kuwa na bima ya kilimo

Je, kuna bima ya kilimo? Kama hakuna. Nini tija ya kuwa na bima ya kilimo

Elvis Legacy

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2017
Posts
3,984
Reaction score
5,820
Nimejaribu kufikiri.

Kutokana na changamoto ya ajira nchini ambapo serikali imeajiri watu wasiozidi milioni moja kati ya watanzania milioni sitini ambapo nguvu kazi ni zaidi ya watu milioni thelathini. Ni wazi kuwa watanzania wengi wamejiajiri au kuajiriwa sekta binafsi zilizo rasmi na zisizo rasmi.

Kilimo kinaweza kuwa moja ya suluhisho la kuongeza ajira kwa vijana kama kitakuwa na uhakika fulani. Vijana wengi wamekuwa wazito kujikita kwenye kilimo kwa sababu ni kama mchezo wa kubahatisha.

Je kuna bima ya kilimo? Kama hakuna ni kwa nini kusiwe na bima ya kilimo? Mfano nalima hekari tano. Kila hekari nalipia bima ya laki moja. Nikifanikiwa kuvuna ni kheri kwangu. Ikitokea kwa bahati mbaya nikapata hasara kutokana na majanga ya asili ikiwemo mabadiliko ya hali ya nchi basi kampuni ya bima inirudishie gharama zote nilizotumia kwenye kilimo ili nianze moja.

NOTE: Kampuni ya bima ya kilimo iwe na wajibu wa kunishauri namna ya kufanya kilimo bora, kuanzia utayarishaji wa shamba, aina ya mbegu, madawa n.k isipokuwa masoko.

Je hili lipo? Kama halipo kuna tija yoyote kuwepo na bima ya kilimo?
 
Kampuni ya bima itafiriska mwaka wa kwanza tu itakapoanzishwa.

Kilimo ni risk sana uwezekano wa kupata ni mdogo kuliko wa kukosa

Ndo maana wakulima wengi ni maskini .

Ndo maana mkulima hakopesheki!!
 
Back
Top Bottom