Je, kuna gharama gani nyingine pale bandarini kwa mtu aliyeagiza gari nje?

border

Senior Member
Joined
Jun 22, 2017
Posts
146
Reaction score
142
Wanajukwaa habari za mchana.

Napenda kujua ukiwa umeagiza Gari nje ni gharama gani nyingine unatakiwa kulipia pale bandarini baada ya Gari kufika bandarini na kulipa gharama za TRA.

Nilikuwa kwenye mchakato wa kuagiza Gari lakini gharama za pale bandarini zijazielewa?

Ahsante kwa ushirikiano
 
Ngoja tusubiri wajuzi wa mambo...

Sina hakika ila mi nimeambiwa gharama itakuwa 950k!
 
Mawakala lazima wakupige kwa kusingizia storage
 
Pale kuna mambo mawili, TRA na Bandari
TRA watakutoza kodi zote kutokana na umri wa gari, ukubwa wa injini, nchi inakotoka, aina ya mafuta n.k.
Pia kuna mambo ya usajili na makabrasha yote.

Tumia hii link kukadiria kodi za gari unayoagiza

Kuna hso bandari nao watakutoza matumizi ya bandari, kuna vi malipo vya ajabuajabu hapo.

Mwisho kutegemea na unatumia agent au utatoa mwenyewe, hapa napo kuna gharama zake.

Ukiachilia mbali malipo ya TRA ambayo yanategemea aina ya gari, kwenye bandari na agent andaa kati ya 600,000/ na 1,000,000/-.

Hizo gharama ni nje kabisa ya zile ulizoagizia gari.
 
Huo mfumo wa TRA nimeishautumia kakadiria jambo na nimeshapata natakiwa kulipia gharama kiasi gani mi sikujua kama kuna Gharama nyingine za Sasa kuna jamaa yangu kaniambia kuna Gharama za TPA, BIMA na masuala mengine madogomadogo na kaniambia TPA tu kwa Gari ndogo ni mil. 1, bima laki 4 nikachoka nakuchoka mi sitaki kutumia mawakala
 
Unaumwa wewe. Nani amekuambia hii kitu kama unaweza fanya mwenyewe. Una kibali cha kuingia bandarini??. Unajua DO. Unajua Shipping line?. Baba hii kazi huwezi fanya. Tafuta Agent
Mimi sitaki kutumia mawakala nataka nifanye mwenyewe
 
Gari ndogo na usipotumia agent itapungua kwa 250,000 ila uwe mzoefu. Haiwezi kufika 1 M.

Bima ni muamala tofauti kabisa unajitegemea
 
Unaumwa wewe. Nani amekuambia hii kitu kama unaweza fanya mwenyewe. Una kibali cha kuingia bandarini??. Unajua DO. Unajua Shipping line?. Baba hii kazi huwezi fanya. Tafuta Agent
Kwani bandarini wanaingia watu wa aina gani
 
Unaumwa wewe. Nani amekuambia hii kitu kama unaweza fanya mwenyewe. Una kibali cha kuingia bandarini??. Unajua DO. Unajua Shipping line?. Baba hii kazi huwezi fanya. Tafuta Agent

Lakini siku hizi chini ya sheria mpya wanaruhusu mtu kutoa mzigo wake bila agent mkuu. Zamani hata iweje lazima utumie agent. Ila kama hauna uelewa wa mambo na uzoefu huo usumbufu wake bora utumie agent tu.
 
Kwa hiyo unapomtumia agent yeye ndio atafanya clearances zote au lazima twende wote mguu kwa mguu?
Yaani kwa mfano Kama total cost ya TRA,TPA na Agent fee ni 5m hizi pesa zote nampa Agent akanilipie au naenda kulipa mwenyewe?
Na hao agents ofisi zao zipo wapi?
 
Hapana mkuu, ni uamuzi wako tu. Gari ikishapakiwa kwenye meli, kuna zile documents na waybill zinatumwa. Unaanza mchakato wa kufanyiwa makadirio ya malipo yako. Hapo itatumika TIN number yako na Kitambulisho cha taifa.

Utapatiwa invoice yenye control number na gharama unazotakiwa kulipa. Unaweza kulipia bank, hapo nashauri kytumia CRDB kwa vile inawahi kuonyesha malipo yamefanyika kwenye mfumo wa TRA, baada ya hapo mtaanza mambo ya TPA sasa wharfage,na takataka ndogondogo na ada yake ya uagent hizo wanakupa wao invoice unawalipa.

Ma agent wapo wengi sana, ni vizuri kujiridhisha na ufanisi na umakini wa agent, anaweza kukucheleweshea mzigo ukaingia gharama za kuhifadhiwa mzigo bandarini.

Lakini akiwa anaielewa kazi yake, meli inaweza shusha gari ikakaa siku moja tu kesho yake iko barabarani.

Kwa ufupi ni makubaliano yenu. Anaweza kufanya kila kitu akakupa tu invoice ya ujumla au ukalipia mwenyewe hasa TRA na TPA akishakupatia control number.
 
Accuracy ya hiyo link kwa gharama ikoje japo kwa kukisia?
 
Sheria mpya imetoka lini
Lakini siku hizi chini ya sheria mpya wanaruhusu mtu kutoa mzigo wake bila agent mkuu. Zamani hata iweje lazima utumie agent. Ila kama hauna uelewa wa mambo na uzoefu huo usumbufu wake bora utumie agent tu.
 
Sawa mkuu Asante sana kwa maelezo yako yaliyoshiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…