Je, kuna Kaza Hukumu katika mirathi?

Je, kuna Kaza Hukumu katika mirathi?

Status
Not open for further replies.

kipapi

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Posts
1,059
Reaction score
1,390
Wanasheria naombeni msaada katika hili, Je kuna umuhimu au ulazima wowote katika kesi ya Mirathi kuwa na "Kaza Hukumu" kama ilivyo katika kesi nyingine zinapomaliza kutolewa hukumu?
 
Hakuna hiyo kitu kwenye kesi za mirathi. Msingi wa kukaza hukumu ni kumlazimisha kwa nguvu mtu alieshindwa katika kesi afanye aliyoagizwa kuyafanya katika hukumu kihiari (alieshinda hufanya kwa niaba) mf. Kubomoa jengo kupitia madalali, kushika akaunti ya alieshindwa ili kupata fedha inayodaiwa, kuuza mali ya mdaiwa ili kupata fedha inayotakiwa kulipwa nk..
Sasa kwenye kesi za mirathi kwa muelekeo huo hakuna cha kukaza maana kunakua hakuna alieshindwa, mtu akishateuliwa kuwa msimamizi basi anaendelea na majukumu.
 
Inategemea shauri la mirathi lililofunguliwa mahakamani Mkuu.

Chukulia kwamba marehemu alikuwa anadaiwa na mtu kiasi cha milioni 15 baada ya kuwaeleza wana familia au msimamizi wa mirathi akagoma kutambua hilo deni ikapelekea mdai kwenda mahakamani kudai haki yake.

Mdai akapata ushindi katika hilo shauri. Halafu mahakama ikatoa amri kwamba mali yenye thamani ya milioni 15 iuzwe ili mdai apewe hela anayodai.

Je hiyo itakuwa ni kaza hukumu au siyo? Kama ndiyo au siyo Kwani?

Pia kama kuna mtu atataka kukata rufaa dhidi ya hiyo kaza hukumu iliyotolewa na mahakama lazima atafuata taratibu za kawaida kama ilivyo kwenye Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Madai(Civil Procedure Code.)

Pia kaza hukumu inaweza kuonekana pale ambapo wanafamilia hawajaridhika na ugawaji mali hivyo wakaamua kwenda mahakamani kutafuta suluhisho. Kwa upande wangu kile mahakamani itakachokisema kuwa mtagawana hivi na vile na kila mmoja atapata hiki hiki hakika naamini hiyo itakuwa ni final decree of distribution of deceased property.

Ni mawazo yangu hayo na unaweza kukosoa nilipokosea. Unapokosoa nahitaji hoja zito zenye mashiko na ushahidi wa kutosha.
 
Kusahihishwa nafikiri ni neno zuri zaidi kuliko kukosoa..

Ulichosema kina mashiko lakini hakipo sawa, najibu haya kwa kujibu hoja mbili ulizoweka kama ifuatavyo
1. Kama mtu anamdai marehemu mpaka ikafikia kwenda mahakamani, shauri litakuwa ni la madai tu (na ili lifanikiwe kusikilizwa lazima kuwepo na msimamizi wa mirathi atayesimama mahakamani badala ya marehemu) na sio la mirathi. Mdai akishinda shauri hilo atakazia hukumu hiyo kesi ya madai aliyokua ameifungua - kesi zote mbili ni za madai tu na sio za mirathi

2. Mahakama haiwezi kuwagawia mali wanufaika wa mali za marehemu, inachofanya ni kumteua (kumthibitisha) msimamizi wa mirathi ambae amechaguliwa na kikao cha ukoo au kuteua adminstrator general kusimamia mali za marehemu kulingana na mazingira yatakavyokua. Ila kabla hajathibitishwa au kuteuliwa na mahakama kuwa msimamizi wa mirathi, inaruhusiwa mtu mwingine kuchalenji uteuzi wa huyo mtu..unaweza kuomba wasimamizi waongezwe au hata wabadilishwe na kuwekwa msimamizi kutoka serikali au hata mtu mwingine tu kama mahakama itaona inafaa lakini uweke sababu za kwa nini unachalenji..lakini mahakama yenyewe haiwezi kugawa mali kwa wanufaika.
Hata hivyo chochote kitachofanyika hapa hakiitwi 'kaza hukumu' ila tu ni mashauri ya mirathi ya kawaida..
Kwa hiyo jibu linabaki palepale kuwa hakuna kukaza hukumu kwenye shauri la mirathi
 
Umejenga Hoja Nzuri Sana!Hongera!
 
Kuna kitu sikielewi kuhusu mirathi... Msaada tafadhari..

Ni nani ana haki ya kupata mirathi ya marehemu hata km hakuorodheshwa kwenye wosia.... Aliouacha marehemu????

Example.

Baba na mama wameacha watoto watatu walifunga ndoa ya kiserikali.

Kuna mali walizovuna woote na kuna mali za mwanaume tu.....

Je mwanaume akifariki, ni nani kati ya mke na watoto ni lazima apate urithi....?

Wat if ikatokea hayuko hata mmoja kwenye wosia, ni nin kinafanyika??

Maaana soon nahisi nakufa kwa hizi tabia za hawa wanangu ni vyeema niandae wosia mali ziende kwa watoto yatima tu...
 
Kukiwa na wosia maana yake wanaorithi ni walioandikwa kwenye wosia na sio vinginevyo, usipofuata matakwa ya mwenye mali (marehemu) kwa kuwapa watu waliopo nje ya wosia halali kunakuwa hakuna maana ya kuandika Wosia.

Ishu za mali za mwanaume tu na mali za mkewe tu, ni mambo ya kuthibitisha mahakamani ikiwa kutakuwa na mgogoro wa mali za urithi, ingawa sheria ya ndoa imeeleza wazi kuwa mali zilizo kwa jina la mwanandoa, bila kujali imepatikana muda gani (kabla au baada ya ndoa) inaaminiwa kuwa ni ya mwanandoa huyo mwenye jina peke yake na sio ya wanandoa wote wawili..ni kazi ya mwanandoa mwingine kuthibitisha kuwa mali hiyo ni ya pamoja licha ya kuandikwa jina la mtu mmoja
 
Kwa iyo kisheria mke hana uwezo wa kudai urithi endapo anakuwa hajaandikwa popote.....
 
Anaweza kudai kwa njia nyingine za kisheria, yaani kitaalamu. Kwa mfano anaweza kudai kwa kusema kuwa mali hiyo iliyoandikwa katika mirathi ni sio ya mrehemu bali ya kwao wote kwa kuwa alichangia na marehemu (uthibitisho utahitajika)

Au kwa kuupinga wosia kuwa haukukidhi vigezo (umeghushiwa, haukuandaliwa kwa usahihi nk)

Angalizo: kama kila kitu kilichoandikwa kwenye wosia ni sahihi, hana nafasi ya kupata chochote..mwenye mali ndiye anayeamua kuigawa mali yake kwa nani..sawa na marehemu angetaka kuiuza kabla hajafa na fedha kuzigawa, kama ni ya kwake wasingemfanya chochote

Kwa iyo kisheria mke hana uwezo wa kudai urithi endapo anakuwa hajaandikwa popote.....
 
Kuna kitu sikielewi kuhusu mirathi... Msaada tafadhari..

Ni nani ana haki ya kupata mirathi ya marehemu hata km hakuorodheshwa kwenye wosia.... Aliouacha marehemu????

Example.

Baba na mama wameacha watoto watatu walifunga ndoa ya kiserikali.

Kuna mali walizovuna woote na kuna mali za mwanaume tu.....

Je mwanaume akifariki, ni nani kati ya mke na watoto ni lazima apate urithi....?

Wat if ikatokea hayuko hata mmoja kwenye wosia, ni nin kinafanyika??

Maaana soon nahisi nakufa kwa hizi tabia za hawa wanangu ni vyeema niandae wosia mali ziende kwa watoto yatima tu...
Acha uchoyo ndugu;Wagawie wote au uza kila kitu kwa njia ya mkopo.Yaani kama ni majengo unayachukulia mkop benki ni rahisi kumanage urithi wa hela kwa sababu ni namba hazidanganyi.Halafu kama kuna nyumba ya urithi ya familia hakikisha unampa mkeo yeye ataamua ampe nani.Ila usiwe mchoyo ukifa wakibaki wanapigana ni kwa ujinga wao
 
Soma teeena uelewe..
 
Anaweza kudai kwa njia nyingine za kisheria, yaani kitaalamu. Kwa mfano anaweza kudai kwa kusema kuwa mali hiyo iliyoandikwa katika mirathi ni sio ya mrehemu bali ya kwao wote kwa kuwa alichangia na marehemu (uthibitisho utahitajika)

Au kwa kuupinga wosia kuwa haukukidhi vigezo (umeghushiwa, haukuandaliwa kwa usahihi nk)

Angalizo: kama kila kitu kilichoandikwa kwenye wosia ni sahihi, hana nafasi ya kupata chochote..mwenye mali ndiye anayeamua kuigawa mali yake kwa nani..sawa na marehemu angetaka kuiuza kabla hajafa na fedha kuzigawa, kama ni ya kwake wasingemfanya chochote
Sheria inamtaka mtoa wosia kurithisha Mali zake na si mali za wengine.
 
Na hakuna anayekataa hilo kuwa huwezi kugawa usichokuwa nacho, ila ungesoma vizuri hoja ya mleta mada kabla ya kutoa jibu lako...

Watu wana mali za ubia lakini marehemu kaigawa kwa mtu mwingine na kutomgusa mbia wake, hajaigawa kwa sehemu yake ya umiliki ila kaigawa yote kana kwamba ni ya kwake pekee, sasa huyu mbia aliebaki anafanyaje kupata mali yake? Ndio moja ya swali la mtoa mada
 
Sawa. Akigawa mali za ubia anakosea sema inampa kuainisha kwenye wosia kuwa sehemu yake kwenye ubia iende kwa flani.
 
Ndio hapo sasa unavyotakiwa kumsaidia ndugu mleta hoja kuwa afanye nini ili aweze kupata sehemu ya mali yake ambayo marehemu kaipoka na kumgawia mwingine

Ila Ikumbukwe pia kuna doctrine ya survivorship, mfano kwa ardhi inayomilikiwa kwa joint occupancy
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom