Akilihuru
JF-Expert Member
- May 20, 2022
- 1,512
- 2,980
Kwema wakuu, mishe zinaendeleaje,
Wakuu kwa wale wakongwe wa miaka ya 80s, bila shaka mtakuwa mnafahamu mchekeshaji huyu ambae alijizolea umaarufu mkubwa kutokana na fani yake ya uchekeshaji yani comedian.
Mzee Jangala alikuwa na timu yake ambayo ilisheheni watu waliokuwa wamebobea katika tasnia hiyo miaka hiyo kama vile mzee Kabunga, Mshamu na wengine wengi ambao nimewasahau.
Sehemu yake kubwa ambayo ilichekesha watu wengi kama sio Tanzania yote, ni kile kipande chake cha mahojiano yeye na mtoto wake (wa kuigiza) alieitwa mshamu. Mahojiano yalikuwa hivi 👇
Jangala: Mshamu hivi siku hizi unakwenda madrasa kweli?
Mshamu: Ndio baba, kwani vipi?
Jangala: kwa sababu nataka kujua unachokisoma huko madrasa.
Mshamu: ah hilo mbona halina shaka mdingi wangu.
Jangala: kweli eeh?
Mshamu: Yes father, tena siku hizi hata kizungu tunafunzwa madrasa.
Jangala anacheka kidogo 😂😂😂 afu anauliza.
Jangala: Sasa hivi uko sura gani?
Mshamu: Nipo ile ile sura ya siku zote uijuayo ya alkariatu. Kuna swali lingine?
Mzee Janganga anakuja juu 😂😂
Jangala: Sasa wewe wenzako kila siku wakienda madrasa wanabadilisha sura, ila wewe kila siku ni alkariatu yani ni kujikalia tu kujikalia tu mshen..z..i mkubwa 😂😂😂😂.
Anamtoa nduki Mshamu anatoka ndugu huku kisigino kinagusa chogo.
Aisee miaka ile tule enjoy sana, pamoja na kwamba nchi haikuwa katika wakati mzuri wa kiuchumi, lkn michezo ile ya Jangala iliwasaidia wengi kukumbuka shida wanazopitia kwa siku kutokana na hali ya maisha.
Anaejua alipo huyu mzee amfikishie salam zake, mwambieni wajukuu zake tunam miss sana. Na kama ashatangulia mbele ya haki basi Mungu ampe pumziko la milele amiin.
Dah enzi hizo Majuto bado yupo kwao Tanga huko hakuna hata anemfahamu.