Hali ni mbaya sana kuelekea kwenye uchaguzi wao serikali za mitaa. Ukiachilia mbali kule kuchezea daftari la wapiga kura kwa:
- Kuongeza majina bbandia
- Kuongeza majina ya waliopotea
- Kuongeza majina ya wanafunzi
- Kuongeza majina ya marehemu na katika ujumla wake kughushi taarifa za hayo makundi yote.
Sasa wamekuja na kituko kingine, Wagombea wa upinzani wa nafasi mbali mbali wameenguliwa kwa asilimia 80.
Bila kutafuta matukio makubwa ya kufunika walau kwa muda madudu ya uchafuzi wao uchaguzi wa serikali za mitaa hali inaweza kuwa mbaya zaidi. Hivyo basi ni lazima kutengeneza matukio makubwa
1. Japo haijathibitishwa ni kwa namna gani iliwezekana lakini tukio la kufungwa Yanga bao 3 kwa moja na Tabora united ni mojawapo.
2. Mkuu wa nchi haonekani, yametengenzwa mazingira ya kumuulizia yuko wapi.
Hii imetoa nafasi kubwa ya kuzalisha mijadala kila kona ya nchi.
Wapangaji wa haya matukio wakiona graph imeshuka watapandisha mengine fasta.
Hivyo basi kuanzia kesho tutegemee kuletewa matukio mapya na yatakuwa ni bandika bandua mpaka uchaguzi upite!