Je, kuna member amewahi kushinda mchongo pesa?

goroko77

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2019
Posts
8,845
Reaction score
13,072
Kila nikisikiliza redio moja nasikia tu watu wakishinda pikipiki na milioni mbili au kashinda milioni tano na bajaji, yaani full kuokota.

Ila sasa ukijaribu kucheki kwa sura nyingine ni kama utapeli unafanywa kwa makusudi na wamiliki wa redio hiyo, kwani mshindi anapigiwa anaulizwa kuwa "Unashiriki Mchongo Mesa, mshindi anasema hapana sijawahi au nilishiriki juzi tu ila leo ndio anakuja kutangazwa mshindi.

Mbna ni uhuni na wizi wa wazi wazi na mamlaka za michezo ya kubahatisha wako wala hatujawahi kuona mshindi akikabidhiwa zawadi zake, huu ni utapeli Clouds FM wanafanya.

Clouds FM acheni utapeli na uhuni, nimeshindwa kuwavumilia. Mnatapeli umma waziwazi, nimechezaa zaidi ya laki tatu sijawahi tangazwa mshindi wala kuonekana mkikabidhi hizo pikipiki kwa washindi.

Kwa kifupi sana, Kusaga acha utapeli na wizi wa wazi, ridhika na hicho kidogo upatacho. Acha wizi haraka sana, vinginevyo rudisha pesa zangu.
 
Ubashiri wa kweli ni mpira tu! We unabet huku watu wanakipiga huko, mwisho wa siku matokeo wote mnayaona! Ukipasuka unapasuka kihalali! Ukiwapasua wanakupa chako, wakizingua unawashtaki maana ushahidi unao!

Achana na michezo ambayo hata jinsi mshindi anavyopatikana haijulikani, ukila hujui umekulaje ukiliwa hujui umeliwaje, utamshtak nan hapo!

Ndo maana wanaweka vinamba vyao hapo katikati wanaweka vi ××× hata mwenye namba hajijui! Utapeli mtupu
 
Nilishinda July 10 kwenye xxl nilicheza mara 3, washindi walikua kumi nami nikawa miongoni mwao laki 5 ikakatwa 15% ya kodi nikatumiwa 425,000/= na jezi zangu 3 nilizochagua
 
Kushinda ni kz kweli kweli alafu wewe ni kutuma pesa tu hata kanuni wanayoitumia haijulikani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…