Hii inatooa changamoto kwa wale watakaokuja kuwa Marais was baadae kuwa wajikite kwenye maendeleo ya watu ili unaporudi kutafuta kuchaguliwa kwa Mara ya pili usipate shida Kama anayopata jamaa. Magufuli ameshindwa kuwashawishi wapiga kura maana kuwatajia kwamba umenunua madege, umwjenga mabarabara wakati watu wanalala njaa na Hali imekuwa ngumu kwa miaka mitano Ni Kama unawapigia kelele. Hivyo Hana Cha maana zaidi ya kupiga magoti na kuomba msamaha kwa wananchi kutokana na mateso aliyowapatia kwa miaka mitano.