Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Suala la kusema kuwa Rais wa WBO hajalipwa haiingii akilini maana mtu hawezi kutoka alipotoka hadi Tanzania kwa ajili ya mechi halafu awe hajalipwa.
Baadhi ya wadau walisema Hassan Mwakinyo ana-ugomvi na watu wengi kwa hiyo wanambania kwa kumfanyia figisu figisu kama hizi.
Je, unadhani ni nani ambaye anaendelea kumbania Mwakinyo hata baada ya kuwa sawa na Azam Media.
Ieleweke kuwa Mwakinyo wakati anapanda alijisahau akaanza kuwa na ugomvi na kila mdau wa ndondi, aliongea vibaya na kuwatendea vibaya baadhi ya watu. Mathalani aliwahi kuwashtaki Azam Media kwa kurusha ile mechi yake aliyosingizia viatu. Mwanasheria wake alimshauri vibaya maana pambano kurushwa hewani sio suala la bondia bali promota.
Hata hivyo kwa Azam kuikubali mechi ya Mwakinyo na Mghana ilikuwa tayari wameyamaliza, yaani Azam asingeweza kukubali kuharibu biashara yake.
Sasa tupeane za kupeana hapa, ni nani anayembania Mwakinyo?