Je! Kuna Siku Binadamu tunaweza Ishi Milele kama Tukiweza Kulila Hili Tunda

Je! Kuna Siku Binadamu tunaweza Ishi Milele kama Tukiweza Kulila Hili Tunda

RGforever

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2011
Posts
6,878
Reaction score
5,432
Ukisoma Kitabu cha Mwanzo katika Biblia Takatifu Mwenyezi Mungu Aliweka Walinzi yaani Malaika Katika Bustani ya Eden ili tu Binadamu asiweze Kula Tunda La uhai maana Akilila Ataishi Milele.

Je Kutokana Na Mwenyezi Mungu kuweka Walinzi Je kuna Uwezekano au Mwenyezi Mungu anajua Kuna Siku Binadamu ataweza Kufikia Mahali hapo na Kulila Hilo Tunda Ndo maana Akaweka Walinzi?.

MWANZO 3:22-24


Kisha Mwenyezi-Mungu akasema, “Sasa, binadamu amekuwa kama mmoja wetu, anajua mema na mabaya. Lazima kumzuia kula lile tunda la mti wa uhai, kwani akilila ataishi milele!” Basi, Mwenyezi-Mungu akamfukuza Adamu nje ya bustani ya Edeni, ili akailime ardhi ambamo alitwaliwa. Alimfukuza nje, na kuweka mlinzi upande wa mashariki wa bustani ya Edeni na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia iendayo kwenye mti wa uhai.

Mwanzo 3:22‭-‬24.


Maswali makuu ninayojiuliza
1. Binadamu tunaweza Ishi Milele kama tukiweza Kula Hilo Tunda?

2. Kwanini Mungu ameweka walinzi? Je! Ni kutuzuia sisi pekee au

3. Je ipi mission ya Hizi Secret society tunazoambiwa Je si kwamba Zinatafuta Njia ya Kuweza Kufika Huo Mti wa Uhai
 
Kutengeneza nadharia kwenye field hii ya kiroho ni kitu rahisi sana. Unaangalia mazingira halisi na unatengeneza uongo ili uendane na mazingira halisi ili watu waweze kuamini. Mimi mwenyewe nina nadharia kibao kuhusu life na vilivyomo ambazo najua ni hekaya tupu bt kuna siku nikizitoa kuna watu watasema nadhatia hizo zinaeleza ukweli.
Hichi kitu kimemtafuna binadamu kwa maelfu ya miaka na kitaendelea kututafuna kwa kuwa sisi tumechagua hivyo.
 
Nani anaejisumbua kufanya upuuzi kama huo wa kutafuta tunda la kwenye kitabu..? watu wako bize kutafuta hela maana hata huko kuishi milele kungefaa nini kama huyo Mungu ameamua kumuachia shetani anaeleta mateso kwa waishio milele..! lkn hata hivyo nikiangalia sababu za kisayansi zina mantiki kuzidi zakidini kuhusiana na kuishi milele na balance of nature.
 
Yesu anasema mm nimi njia kweli na uzima.
Pia kwenye ufunuo analindwa na makerubi ambao kule kwenye kitabu cha mwanzo wanaulinda mti wauzima.
Na huo mti wa uzima mmiliki wake ni mmoja, hakuna mwanadam awezae kuufikia isipokuwa kupitia yesu kristo

Ile miti miwili ilikuwa ni watu si ma apple.
 
Yesu anasema mm nimi njia kweli na uzima.
Pia kwenye ufunuo analindwa na makerubi ambao kule kwenye kitabu cha mwanzo wanaulinda mti wauzima.
Na huo mti wa uzima mmiliki wake ni mmoja, hakuna mwanadam awezae kuufikia isipokuwa kupitia yesu kristo

Ile miti miwili ilikuwa ni watu si ma apple.
Mkuu hapo mwanzo umesema yesu ndio mti wenyewe na sasa hivi unasema huo mti hakuna mtu atakayeufikia huo mti isipokuwa yesu, kwa hiyo yesu sio mti tena bali ni njia ya kwenda kwenye huo mti, na huko mwanzo tumeambiwa hakuna mtu anatakiwa kuufikia huo mti kwa kuwa akiufikia na kula tunda ataishi milele. Kwa maana hiyo yesu ni njia ya kuelekea kule ambako Mungu alishakataza. Unavuruga vuruga mambo.
 
Inawezekana kabisa ila tatizo ni moja lile tunda liko Eden ya zamani kwa saiz hatuwez kulipata maana kama ule mti ungekuwepo watu wangetafuta njia ya kwenda kuiba hata kama kuna walinzi
 
Back
Top Bottom