Je, Kuna Taasisi ya ovyo Kabisa Nchini Kuizidi TANESCO?

Mm nachoshangaa ivi kweli think tank ya CCM yote wakaona wachome pesa za kodi za watz maskini ili msafara wa mwenezi upite nchi nzima kufanya zile drama za kupanda punda???real???wananchi wanalia umeme hakuna nchi nzima halafu mna waletea drama kama zile???kweli hii nchi tumerogwa aisee
 
Wewe unasema ya hovyo wao wanaiba mabilioni ya hela za walipa kodi na misaada ya kutembeza bakuli kila kona
Umeme gani usiowaka miaka na miaka kama sio wizi wa kijinga
Mbona nguzo tunaziona kwa wenzetu zinapita mpaka kwenye maji ya kina lakini zinahimili
Kwa sababu hela za zege wanapitia maama haiwezekani eti kila leo sababu ooh zimeanguka kwa sababu ya mvua

Angalia mpaka madaraja, kweli daraja liko urefu sawa na binadamu mnaliita daraja
Tunaendekeza sana wizi kila mahali ndio maana
 
Nakubaliana na hoja. Pia hii ni zao la uongozi mbovu kupita yote ya ccm tangu tupate uhuru.
Kwa nini nasema hivyo, alie ingia alituaminisha kuwa anafuata nyayo za mtangulizi wake. Lakini alichofanya ni kupiga U turn ya nguvu. Kwanza akafuta umeme wa sh.27,000 na kumfulumusha waziri wa mtangulizi wake, kuhakikisha hili wazo linapotea kabisaaa....
Kagundua hicho too late ndio anatuletea cheo cha kisiasa kutupoza(naibu waziri mkuu kutoka kona ile ile). Kakamua wananchi badala ya kulipa 27 kuingiziwa umeme sasa lazima uanze na 350000. Lengo ni kuhamisha pesa zipatikana kwenda kuwalipa wenye vyeti feki waliorejeshwa makazini na -mafisadi wapya wanaokula kwa urefu wa kamba zao. shikanoo ccm

cc lucas mshamba njoo uniprove me wrong
 
We tatizo hapa ni maamuzi ya matumizi ya pesa za kodi zetu kuvurugwa.
Magu aliamua kurekebisha hii kitu (upatikanaji wa nishati ya umeme) ili kuimarisha uchumi, aliweza hili kwa kutoongeza misharara(mfano) ili baadae aongeze wakati huo bwawa la umeme liwe limekamilika. Asingekufa nauhakika kabla hajamaliza awamu zake angefaulu. Sasa dada yako kaingia kaona achote pesa akaongeze mishahara ili asifiwe, matatizo yalianzia hapo. Matokeo yake ndio haya mradi wa umeme unayumba mazima na kuua uchumi wa nchi. Nimetoa mfano 1 wa namna maamuzi ya ovyo yaliofanywa na awamu hii. Kukurupuka eti ndio unaleta cheo cha siasa serikakini kuwapoza watu wasipaze sauti. Nawaambieni Teuzi zozote dakika hizi za lala salama ni mbio za mfa maji. Ni sawa na timu ya mpira iliyofungwa gori 5 inaanza kuingiza wachezaji wapya dakika za majeruhi- kuna mambo yatazidi kuyumba kwa hizi pangua pngua hasa pesa zilipelekwa siko na plani ya mtangulizi wake. Hapa tunaongelea tanesco tu, kjuna nyingine zipo ambazo uhuni huu unafanyika, kubwa kuliko bandari ambayo madhara yake ni chini kwa chini sio kama hili ambalo maumivu yake ni papo kwa papo.
Mlinzi wa mipaka keshadokeza kuna wasiostahili wanatuamulia mambo, sasa msitake tuongee ya uvunguni endeleeni kulala!

cc; chawa wote akiwepo lucas prove me wrong
 
Yawezekana hakuna!
Tatizo 99% ya taasisi za serikali ziko HOVYO!
Kufanya kazi kwa mazoea..
Nidhamu, ukiritimba, uvivu, hawako creative katika uboreshaji wao wa kazi, hawataki mabadiliko ya aina yoyote kufanya kazi yao iwe rahisi na kumsaidia raia...
Sababu ya kutokuwa na performance review na targets basi wanaingia job na kutoka watakavyo, bila uwajibikaji wa aina yoyote ile!
They are just LUCKY PEOPLE KWA KULIPWA MISHAHARA BILA PRESSURE YA AINA YOYOTE ILE!
 
Nchi ya hovyo,viongozi WA hovyo,wananchi WA hovyo angalia bei ya sukari inavyopanda Kwa Kasi ivi Sisi tumelogwa na Nani?ili tumtafute uyo alietuloga atuzindue alafu tunaposema haya Hao waliopo madarakani wanajifariji Kwa kusema Hao wanaoongea hivi Ni wapinzani.
Hakuna mpinzani wala nini Sisi Ni watanzania ambao hatuna vyama,tunaona madhara makubwa ya kukosekana Kwa umeme vijana wengi wamejiajiri kwenye shughuli mbalimbali zunazotegemea umeme Leo hii unakata umeme masaa 12 ivi hawa watu Wana hata chembe ya uchungu Kwa watanzania wenzao?.
Umeme unapokatika shughuli za uchumi zinasimama na wenye uwezo kidogo watajitahidi kununua mafuta na kupelekea kuzalisha Kwa gharama kubwa na kusababisha mzigo mkubwa Kwa mraji WA mwisho.
Hii kitu haivumiliki ningekuwa mm Rais nafukuza Kazi viongozi wa Taifa,Mkoa mpaka Wilayani mana huu Ni upuuzi nchi IPO gizani wananchi wanateseka alafu Kuna watu wanalipwa mishahara na maposho na Magari juu wanayaona haya lkn hawachukui hatua.




Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
 

Tatizo lipo kwa kiongozi mkuu. Yeye ndio anatakiwa awe na ujasiri wa kuminya kitufe kule juu bila kuogopa kilio cha ndugu flani ovyo hapa chini. Ndio mjue nani anastahiki kukaa pale.
Tatizo mama ni katiba hususani mfumo mzima wa kumpata na kumzibiti huyu kiongozi mkuu ili aee kayika kiwango stahiki kwa level yake na izito wa majukumu yakd
 
Rais wa awamu ya 2 aliwahi kusema,
namnukuu...

"Kila zama na kitabu chake"

maana yake kila jamii, jumuiya au familia ina utaratibu wake wakufanya mambo yake...
Huwezi tamani uwe na familia ya watoto 10 kama ya Fulani wakati ata kupata mtoto 1 huwezi kuzalisha 🐒

Relax,
Wizara ilishaeleza nini tatizo, Rais alishatoa maagizo na maelekezo kwenye hili, muhimu ni kuwa na subra,wastahimilivu na wangwana.

wakubwa zenu waliwaelekeza mfanye maandamano juzi hili hawakuliona la muhimu kwasabb wanajua linashughulikiwa....

kama umenena yote hayo ili kutoa dukuduku la moyoni na kupata relief, well and good nadhan uko sahihi kabisaaaa, big up sana 🐒
But issue inashughulikiwa na bilashaka unajua...
 
Nakubaliana na hoja yako.
Pamoja na kuwadiss tanesco, tunapaswa kujiuliza pia: Hivi kuna eneo lolote angalau moja ambalo sisi kama nchi tunafanya mambo kwa ufanisi na weledi?
 
Tatizo nchi yetu, Raia tunalalamika, utakuta kiongozi mkubwa naye analalamika. Tanesco kinachowasumbua wanatumika sana kisiasa, ilibidi watolewe kwenye monopoly waruhusu ushindani kutoka makampuni binafsi.
 
Hivi ni lini TANESCO walitoa sababu za kukosekana kwa umeme na wakasema matatizo hayo yataisha lini, halafu ikawa kama walivyosema?
 
Hivi ni lini TANESCO walitoa sababu za kukosekana kwa umeme na wakasema matatizo hayo yataisha lini, halafu ikawa kama walivyosema?
kua mstahimilivu na mwenye subra hivi karibuni tu marekebisho yanayofanyiwa kazi yakikamilika changamoto hii itakua imeisha...
 
Sioni kama tatizo linashughulikiwa, labda useme kuna watu wanahangaika, kwa maana anayehangaika siyo lazima akuletee matokeo chanya.

Mathalani mtu mjinga asiyeelewa anaweza kuuangusha mti mkubwa kwa njia gani, anaweza kuwakusanya wajinga wengine akawaambia wasukume mti mpaka uanguke. Watasukuma asubuhi mpaka jioni, leo hadi keshokutwa, lakini mti hautaanguka. Hawa wanahangaika, hawashughuliki kuuangusha mti.

Tangu 2021 TANESCO na Wizara wanasema kuwa wanashughulika, na kuweka ahadi nyingi za kutatua tatizo, lakini kila siku tatizo linazidi kuwa kubwa zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…