Je, kuna ubaya gani TRA wakifungua biashara Kariakoo kwa muda wa mwaka mmoja ili kujua namna ya kuboresha sera za kikodi?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Binafsi naamini ni ngumu kwa TRA kuelewa hali halisi inayolalamikiwa bila kufungua duka la majaribio Kariakoo.

Walipe Kodi zote stahiki, na wasiuze chochote bila kutoa risiti, watoe risiti na wadai risiti kila wanaponunua. Wasijipe upendeleo wa aina yeyote na wasitoe rushwa, halafu tuone kama mwaka unaofuata hawatafunga duka.

Pia, Soma=> Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024
 
Binafsi naamini ni ngumu kwa TRA kuelewa hali halisi inayolalamikiwa bila kufungua duka la majaribio Kariakoo.

Walipe Kodi zote stahiki, na wasiuze chochote bila kutoa risiti, watoe risiti na wadai risiti kila wanaponunua. Wasijipe upendeleo wa aina yeyote na wasitoe rushwa, halafu tuone kama mwaka unaofuata hawatafunga duka.
Daah hii imekaa
 
Chanzo kikubwa Cha mapato ya serikali ni kukusanya Kodi, Hawa wanaoruka Kila siku kiguu na njia kwenda kufata mikopo ndo wanatuua kabisa, ikifika muda wa kulipa hawana namna zaidi za kumkandamiza mwananchi kupitia Kodi ili warudishe pesa za mikopo

Huu ni mwanzo tu, kwa wanachofanya huyu mama na Mzee wa singida we subiri baada ya miaka mitano tutalia na kusaga meno
 
Kwa sasa tunalipa mikopo na riba zaidi 50% ya makusanyo, ni kama Trillion 12 hivi tunawalipa riba mabeberu kila mwaka!
 
Hilo duka liwe la bidhaa gani. Nguo au electronics au plastic maana pale Pana biashara nyingi ukisema wafanyabishara wengi wengine hawapati faida nakataa
 
Back
Top Bottom