Tetesi: Je, kuna ufisadi kwenye taasisi za Serikali zisizohudumiwa na NHIF

Tetesi: Je, kuna ufisadi kwenye taasisi za Serikali zisizohudumiwa na NHIF

tutafikatu

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2011
Posts
3,327
Reaction score
4,624
Ninashangaa sana kuona taasisi za Serikali kama BoT, SUMATRA, TANESCO n.k. wafanyakazi wake hawajajiunga na Bima ya Afya ya Taifa.

Wengine wanasema yamkini pesa zao za matibabu zinapigwa sana. Mwingine alidai kuna 10% wanaipata viongozi wa baadhi ya taasisi toka private health insurance firms.

Kwa TANESCO huduma zao za matibabu ziko hovyo na complicated.

Ajabu hata JWTZ hawako NHIF wakati hospitali zao hazijitoshelezi.

Kuna harufu ya ufisadi kwenye hili.
 
Mkuu umenena point ya msingi sana.Naomba ipate wachangıaji na wasomajı wa kutosha JPM hajajua.
 
Mkuu umenena point ya msingi sana.Naomba ipate wachangıaji na wasomajı wa kutosha JPM hajajua.
Kwa kweli inashangaza sana kuona taasisi kama Tanesco zinaingia mikataba na hospitali binafsi halafu baadaye fomu za madai zikapitiwe na kampuni kama AAR. Kwanini wasijiunge kwenye taasisi ya kiserikali ambayo imejitpsheleza kabisa. Kuna kitu hapa.
 
Jamani Kuna utaratibu ndani ya sheria kupata mtoa Huduma kwa kushindanisha watoa Huduma huwezi kufanya single sourcing km Kuna watoa Huduma Sokoni. NHIF yawezekana haishiriki ktk hii michakato kwa kubweteka au haikidhi vigezo.
 
Unashindanisha nini mkuu?

Unataka useme BoT waliwapata Jubilee Insurance baada ya kuwashindanisha na Strategis, Metropolitan, na watoa huduma wengine?

Unataka kusema TANESCO inashindanisha hospitali inazoingia nazo mikataba ya kutibu wagonjwa wake? Kwanini wahangaike kuingia mikataba na hospitali moja moja, halafu fomu za madai wazipeleke AAR ili zikapitiwe? Huu mlolongo unapunguza au kuongeza gharama? Mbona pesa zenyewe za matibabu wanazodaiwa na hospitali wanatoa kwa manati?
 
Back
Top Bottom