Je kuna uhalali wa kiasi gani kwa mwajiri kukata mshahara wa mfanyakazi kwa madai ya kutofanyika kwa retirement.

Jadong

New Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3
Reaction score
0
Wakuu kwanza nitangulize shukrani zangu hasa unapofikiri kunipatia msaada katika hili.
Kuna kampuni moja kubwa tu hapa kwetu ila kitu kinachosikitisha ni namna inavyohusiana na wafanyakazi wake hasa katika maslahi yao, ila kubwa ninalohitaji msaada kwenu ni kutaka kujua kwamba sheria ya kazi imetoa mianya kwa kiasi gani kwa muajiri kukata mshahara wa mfanyakazi kwa madai ya kwamba fedha ya matumizi ambayo ofisi imekupatia japo matumizi uliyafanya tumeyaona ila Retirement (mrejesho wa matumizi) yako hatujaona hivyo tunakata mshahara wako.
Sasa hapa ofisini imekuwa kama ni njia moja wapo ya kuongeza mapato ya kampuni kwa njia hiyo.
Tafadhari nimezungumza kiufupi sana kimsingi shida haiko kwa wafanyakazi bali shida iko kwa wakuu wenyewe so niombe nisaidie tu kujua Jinsi gani sheria ya Kazi imewapa mianya wakuu wetu kukata mishahara wakati wowote wanapojisikia kwa kigezo cha retirement?
 
Hyo kawaida..
Inakuaje unapewa ela za ofisi alaf unazitumia kama mshahara wako
 
Hebu kwanza fafanua unamaanisha nini kusema kuwa matumizi wameyaona, ila hakuna mrejesho wa matumizi.

Pesa za kampuni si zakuchezea. Kukukata mshahara kwanza wamekuhurumia
 
Utaratibu uko vipi hapo kwenu kuhusu uchukuaji na urudishaji wa retirement? I mean unatakiwa ufanye retirement ndani ya siku ngapi toka umalize /kufanya matumizi ya ile pesa?
 
Hyo kawaida..
Inakuaje unapewa ela za ofisi alaf unazitumia kama mshahara wako

Yaani mkubwa point ni kwamba retirement ulizifanya ukawasiwasilisha kwa wahusika (watu wa account) then baada ya mwaka wewe unajua uko katika mazingira salama leo unaona jina lako kwenye orodha ya watu wanaodaiwa hizo imprest na wakatika unajaribu kukusanya dondoo zinazoonesha kwamba ulifanya retirement mshahara umekwisha ingia na umekatwa na wakati unacross check na watu wa fedha wanabaini kweli walizi-misplace au walizipoteza so kosa hapo lilikuwa kwao lakini pesa ndo ishakatwa.
(Du kama ni kitu cha kawaida hapo kuna watu watakuwa hawafanyi wajibu wao wakijua wao hawapatwi na baya lolote. Asante kwa muda wako mkuu)
 
Hebu kwanza fafanua unamaanisha nini kusema kuwa matumizi wameyaona, ila hakuna mrejesho wa matumizi.

Pesa za kampuni si zakuchezea. Kukukata mshahara kwanza wamekuhurumia

Nachomaanisha kwamba matumizi wameyaona ni kwamba mfano umeomba pesa kama allowance wakati walimu wanasahihisha mitihani na kila mwalimu anajua idadi ya scripts alizosahihisha na siku alizotumia so mnaomba jumla kuu walimu wanasahihisha na kupewa pesa zao nao wanatoa matokeo kwa namna yalivyosahihishwa na mnayakusanya nakuwatumia wakuu. Ni mfano wa scenario hiyo ndio nilokuwa namaanisha mbali ya mambo mengine.
 
Hapo wamekosea. Kwanza ulitakiwa kusaini kuwa umeridhia kukatwa mshahara
 
Back
Top Bottom