Je, kuna uhusiano wa taa ya Engine na steering wheel hydraulic?

Kaka Kapo

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2012
Posts
547
Reaction score
344
Wasalaam wataalamu.

Aisee nina ki-gari changu aina ya Chevrolet Optra Lt 2.0 hivi majuzi kimeanza ku-misbehave kina washa taa ya Check Engine halafu kinanakuwa kizito kuchanganya mfano ninapokuwa kwenye foleni muda wa kuondoka kinachelewa.

Nikapeleka kwa dignosis kikarusha code P0700 nimefanya research inaonesha hiyo code ina trigger na shida nyingi ikiwemo transmission fluid either ikiwa low au imeingua wanasema wataalamu.

So baada ya ku-diagnose tuli-clear ile code jamaa akanishauri nifanye service ya gear box kwa kubadili transmission fluid so nikaendelea kutumia gari huku najipanga kwa ajili ya kufanya hiyo service.

Sasa juzi ile taa ya check engine imerudi tena leo nikafungua boneti kucheki maji na routine checks kabla sijaondoka nikagundua hydraulic ya steering wheel imepungua nikaongeza nawasha gari ile taa ya check engine imeindoka na gari inapiga kazi vizuri.

Swali langu ni je kuna uhusiano wa taa ya engine na steering wheel hydraulic? Wataalamu naomba kuelewa hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…