Areus
JF-Expert Member
- Jul 27, 2016
- 337
- 417
Habarini JF members, poleni na majukumu lakini pia hongereni kwa kuendelea kufuatilia kampeni zinazoendelea nchini kuanzia tarehe 28/8/2020.
Nimeleta mada yangu kwa muundo wa swali ili kujaribu kufanya uchambuzi kidogo kampeni zinazoendelea nchini hasa macho na masikio ya watanzania wengi Ni kutaka kuona na kusikia mtitiriko wa hoja za ahadi kwa KIPINDI kijacho cha miaka mitano, hasa kwa wagombea wawili wa chama tawala Chama cha Mapinduzi (CCM) ndugu Dr John Pombe Magufuli na Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ndugu Tundu Antipas Lissu.
Nimeona watu wameshaanza kuaminishana juu ya idadi ya watu waliohudhuria kwenye kampeni na uhusiano wake kwenye matokeo yatakayotokana na kura zitakazoenda kupigwa mwezi October 2020. Watu wamebeza ufunguzi wa kampeni za Chadema na kudai idadi ya waliohudhuria ni kidogo hivyo hawezi kushinda uchaguzi, Lakini pia mahudhurio ya watu kwenye ufunguzi wa kampeni za CCM pale Dodoma ni makubwa Kwahyo ni ishara tosha ya matumiani kuelekea October 2020.
Hilo kwangu mimi haliwezi kunipa hitimisho ya kuamini kuwa idadi ya waliohudhuria kwenye kampeni Kama ninkubwa Basi inaleta matumaini na kama Ni ndogo Basi haileti matumaini kuelekea October 2020.
Kwanini?
Siwezi kuamini kwamba kuna uhusiano wowote Kati ya idadi ya watu kwenye kampeni na kinachotokea baada au matokeo ya uchaguzi yanavyototangazwa na Tume ya uchaguzi. Kwasababu ya ulinganishinwa kampeni za mwaka 2015 kati ya mgombea wa UKAWA mheshimiwa Edward Lowasa na mgombea wa CCM mheshimiwa John Pombe Magufuli. Lowasa aliweza kuwa na influence kubwa na kampeni zake kuongoza kwa kuwa na watu wengi kuliko hata mgombea wa CCM kwa Kipindi hicho. Hiyo iliaminisha watu kuwa Lowasa angeweza kushinda uchaguzi kwa kile alichokiita Watu kuwa na mahaba na yeye Kwenye kampeni zake.
Lakini matokeo yalikuwa tofauti na idadi watu waliokuwa wanamsikiliza kwenye kampeni zake tofauti na mgombea wa CCM. Kwahiyo hapo ndipo nilipoamini hakuna uhusiano wa moja kwa moja Kati ya idadi ya waliohudhuria kwenye kampeni na kinachotokea kwenye sanduku la kura. Kwahiyo tusipende ku-judge na kutumia idadi ya watu ku-justify matumaini ya ushindi.
Madhara yake ni nini?
Ni kutokukubali pale matokeo yanapotangazwa kama mgombea ameshindwa, hivyo kupelekea vurugu na vitu vingine.
Watanzania 80% hatuna uwezo wa kusikiliza sera za wagombea zaidi ya kuwa influenced na vitu ambavyo sio vya msingi, hatuna uwezo wa kubadilisha mawazo ya kuchagua wakati mgombea akiwa jukwaani akinadi sera, ila tunatembea na ya kwetu moyoni, chama damu damu hata kama sera zake zikiwa hazina mashiko kwa mustakabali wa Taifa letu, siku ya siku ninkuchagua tu aidha uliye kuwa naye moyoni mwako au wa chama chako damu damu. Hapo ndipo unapokosekana uzalendo wa kweli.
Nimejifunza sana siasa za mwaka 2015 ndio maana siwezi kutabiri nani ataibuka kidedea.
Maendeleo hayana vyama