dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,502
- 3,483
JE, KUNA UKOMO WA IDADI YA MAKOSA UNAYOTAKIWA KUANDIKIWA KWA SIKU AU KWA MARA MOJA NA ASKARI MMOJA?
Huenda ni swali linalokusumbua mara kwa mara. Jibu la swali hili ni HAPANA hakuna ukomo. Askari mmoja katika point moja anaweza kukuandikia makosa hata 10 kwa mara moja ili mradi tu makosa hayo yote yanajitegemea, mfano:
Kutokuwa na leseni au kuendesha na leseni iliyosiha muda wake
kutosimama kwenye zebra
kutokuwa na riflekta
ubovu wa gari, mfano tairi au bodi au brake au taa
gari kutokuwa na bima
kutokuwa na kadi ya gari
kuendesha ukiwa na kilevi kuzidi kiwango kilichowekwa kwa mujibu wa sheria
kuzidisha mwendo
Ukikutwa na makosa haya kisheria askari ana haki ya kukuandikia faini zote 8 ili ulipe 240,000 au akaamua kwamba una makosa mengi mno wewe ni wa mahakamani tu.
Na Je, vipi kuhusu kurudia kuandikiwa?
Hakuna popote katika sheria panapomzuia askari mwingine kukuandikia kosa lile lile uliloandikiwa sehemu nyingine. Mfano ukiwa Gairo ulipigwa tochi umezidishwa mwendo askari wa Gairo akakuandikia, ukafika Pandambili ukapigwa tochi nyingi umezidisha mwendo askari huyo wa pandambili atakuandikia tena.
Kisichotakiwa na sheria ni kumwandikia dereva makosa mengi kwa kosa lile lile Mfano gari imekaguliwa ikakutwa na taa mbovu, bodi chakavu, brake hazishiki vema, wepa hazifanyi kazi. Haya sio makosa manne (4), bali hilo ni kosa moja tu ambalo ni ubovu wa gari na faini yake ni 30,000 au mahakamani 50,000 kama ilivyo katika kifungu cha 39(5) cha RTA. Aidha, ikiwa utakuwa umevuka taa nyekundu askari akuadhibu kwa kosa hilo na sio kosa la kutoheshimu ishara na alama, na wakati huo huo akaandika failure to comply with road traffic kinyume na section 113 (kosa na.23).
Ni matumaini yetu umeelewa.
Credit: RSA Tanzania.
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote.