Je kuna ulazima wa kupiga ribiti kwenye gari?

mlinzi mlalafofofo

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2008
Posts
725
Reaction score
1,282
Wakuu kuna jamaa yangu ameingiza mkweche (gari) kutoka kwa mjapani. Sasa kuna wananzengo wanampiga saundi eti apige ribiti kwenye maeneo mbalimbali ya gari kama vile kwenye taa na maeneo mengine yaliyo loose eti ili wajuvi wasipate tamaa ya kuvikwapua vitu ivo.

ivi wakuu kuna ukweli ktk hili au ndo muendelezo wa sanaa na janjajanja za mjini watu wanataka watokemo kupitia huyu jamaa yangu?

mm nimemshauri asiweke maana naona kama ni uharibifu tu ndo unaofanyika pale maana wanatoboatoboa gari kila sehemu na kuiacha gari ina mashimo ya milele.
 
Ushamba tu ule. Bora kuandika namba kwenye vioo.

IMG_0537.jpeg

Siweki na sijawahi kuweka izo kitu.
 
Wakuu kuna jamaa yangu ameingiza mkweche (gari) kutoka kwa mjapani. Sasa kuna wananzengo wanampiga saundi eti apige ribiti kwenye maeneo mbalimbali ya gari kama vile kwenye taa na maeneo mengine yaliyo loose eti ili wajuvi wasipate tamaa ya kuvikwapua vitu ivo.

ivi wakuu kuna ukweli ktk hili au ndo muendelezo wa sanaa na janjajanja za mjini watu wanataka watokemo kupitia huyu jamaa yangu?

mm nimemshauri asiweke maana naona kama ni uharibifu tu ndo unaofanyika pale maana wanatoboatoboa gari kila sehemu na kuiacha gari ina mashimo ya milele.

Muhimu maana mateja wanang'oa chata(brand) ,wang'oa power window,rain guards etc....
 
Wewe mtoa mada mwambie huyo jamaa yako aende akaweke ribiti fasta sanaaa.
Hakuna MTU anapenda kuharibu gari yake Kwa kuweka ribiti ila hakuna namna kutokana na wezi.
Mimi nipo kariakoo miaka mingi pamoja na u-legend wangu bado jamaa waliiba mkanda Fulani upo juu ya paa ya gari....ingawa niliupata baadae lkn nilitoa pesa mwisho wa siku
 
Hata usijali mkuu. Ila siku vibaka wakichomoa kioo cha side mirror kwenye foleni, na hawezi kuacha gari kukimbiza mwizi, mje hapahapa, tutawaelekeza wapi mtaipata kwa bei nafuu kabisa.
 
Kuna maamuzi mengine tunafanya kwa kuangalia usalama tu.

Mara nyingi yanakuwaga sio rational lakini reasonable.

Ni kama tu mwananchi siku moja ainuke kusema kitu rational kabisa "Oya eeh tuachane na kulilipa jeshi hela wala kulijali, tunaingia gharama bure bora tungelimia alizeti". Ni rational kabisa lakini mwananchi yeyote mwwnye akili timamu atakujibu ACHA UJINGA.

Kwa hiyo nwe weka tu, na kama haupendi kuharibika muonekano, basi ndio wakati sasa wajasiriamali wabuni mbinu ya kuimarisha bila kutoboa na ma rivets.
 
Wewe mtoa mada mwambie huyo jamaa yako aende akaweke ribiti fasta sanaaa.
Hakuna MTU anapenda kuharibu gari yake Kwa kuweka ribiti ila hakuna namna kutokana na wezi.
Mimi nipo kariakoo miaka mingi pamoja na u-legend wangu bado jamaa waliiba mkanda Fulani upo juu ya paa ya gari....ingawa niliupata baadae lkn nilitoa pesa mwisho wa siku
duuh kweli kuna umuhimu kuweka iyo kitu aisee
 
Wakuu kuna jamaa yangu ameingiza mkweche (gari) kutoka kwa mjapani. Sasa kuna wananzengo wanampiga saundi eti apige ribiti kwenye maeneo mbalimbali ya gari kama vile kwenye taa na maeneo mengine yaliyo loose eti ili wajuvi wasipate tamaa ya kuvikwapua vitu ivo.

ivi wakuu kuna ukweli ktk hili au ndo muendelezo wa sanaa na janjajanja za mjini watu wanataka watokemo kupitia huyu jamaa yangu?

mm nimemshauri asiweke maana naona kama ni uharibifu tu ndo unaofanyika pale maana wanatoboatoboa gari kila sehemu na kuiacha gari ina mashimo ya milele.
Kuchafua tu gari
 
Back
Top Bottom