Je kuna ulazima wa kusoma Falasafa na elimu ya Mantiki,ili niweze kuhoji mambo vizuri na kuwa na hoja thabiti ?

Kisai

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Posts
28,481
Reaction score
28,749
Naanzia hapa :

Tangu nakuwa nilikuwa nasikia kuhusu Falsafa na wanafalsafa,mantiki na watu wa maneno.

Maswali kadha wa kadha nikawa najiuliza na mpaka muda huu najiuliza. Rejea kicha cha habari hapo juu.

Je ili nionekane mtu makini katika hojaji na mitazamo iliyopevuka je kuna haja ya kusoma elimu hizo mbili ?

Je kuna haja ya kusoma Falsafa na elimu ya mantiki ili niupate ukweli ?
 
Tilia moazo na maanani kila unachotakiwa au kuamua kujifunza. Kielewe vizuri ki ufasaha. Vilevile unaweza usiwe mtaalam au uelewe mambo yote, chagua eneo moja zama na bobea huko.
 
Sasa kwa sisi tulioishia la saba[emoji37]

Hata hilo neno lenyewe falsafa hatuliju.!

Na kwanini watu waite icho kitu falsafa hatufahamu.!

Hivi kama hutojali unaweza kutupatia maana kwanza ya neno lenyewe.?

NB: hiyo inayoitwa kuzungumza kwa mantiki kanuni zake ni zipi.?
 
mimi nilidhani falsafa ni natural born with trait
pia unaweza kuidevelop from within kama ukiamua kuipenda,

mimi naamini kila mtu anao uwezo wa kufikirisha ubongo wake na kujenga hoja zilizosimama vizuri na kuweza kuzisimamia ipasavyo,

falsafa ni elimu, tatizo moja nimeliona kwa vijana wanaowasoma wanafalsafa ni kutaka kuwa na msimamo/falsafa kama za mwanafalsafa fulani, wanashindwa kuelewa yeye alikuwa vile sababu ya hali aliyokuwa nayo au mazingira aliyopitia,

ubongo wa mwanadamu unauwezo mkubwa sana....watu hawataki kuutumia vizuri.
 

Philosophy is a combination of 2 Greek words, Philo and Sophia, i.e Friend and Wisdom, therefore Philosophy is a study of wisdom or love of wisdom. The Language of Philosophy is Logic and Logic is both Word and thought, Logic is both a science and art. You need to have a thought and that thought need a language to be expressed or communicated.

There are other branches of Philosophy Metaphysics - the study above the pyhysics, Cosmology - deals with the cosmos, Epistemology - deals with ontological truth etc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…