Je, kuna umuhimu wa mapinduzi ya viwanda nchini Tanzania?

Je, kuna umuhimu wa mapinduzi ya viwanda nchini Tanzania?

Bruno William

Member
Joined
Jul 24, 2022
Posts
6
Reaction score
3
HISTORIA FUPI YA MAPINDUZI YA VIWANDA

Nchi nyingi duniani zilizo endelea zimepitia mapinduzi ya viwanda, na mapinduzi hayo yalihusisha hatua, michakato na pia hatima mbalimbali ambazo zilipelekea nchi nyingi barani ulaya kafanya maaumuzi tofouti tofauti ili kukidhi uhitaji wa viwanda ambavyo teyari vinaanzishwa,vilisha anzishwa. Mapinduzi ya viwanda yalinza rasimi miaka ya 1760's ambako yalikuja baada ya mapinduzi ya kilimo na kuondoa ufanyaji wa kazi kwa mikono kuenda kwa njia ya mashine na mpaka leo hii dunia inaendelea kuboresha namna kazi zinavyo fanywa kwenye viwanda mbali mbali.

Miaka ya 1885 ili saidia nchi nyingi duniani kujikusanyia mali Katika bara la Africa kwa njia ya kujigawia kila mtawala mkubwa duniani na kutengeneza mipaka ya nchi mbali mbali barani Africa hivyo kurahisisha upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda vyao. Pia vipo viwanda ambavyo wali vianzisha barani Africa na kuua vile ambavyo walivi kuta kwa ajili ya maslahi ya viwanda vyao na kudhoofisha uchumi wa viwanda vidogo vidogo barani Africa. Si suala geni kusikia Tanzani kulikua na viwanda lukuki lakini sasa yamebaki magofu tuu!!

Je, YAPI MAHITAJI YA VIWANDA
1. Rasiliamali watu- Hakuna kiwanda ambacho anzishwa, kuendeshwa bila kuwa na rasiliamali watu ambao ni muhimu kwa ajili ya shughuli kama usimamizi, uendeshaji wa mashine, usafi, ubebaji wa malighalifi na pia bidhaa zilizo zalishwa. Ni muhimu kuwa na watu wenye uzoefu pia na taaluma mbalimbali zinazo endana na aina ya bidhaa lengwa zinazo zalishwa, wataalamu wa kupima ubora, wasimamizi wa fedha na maudhui ya kiwanda.

2. Malighalifi kwa ajili ya uzalishaji- kila kiwanda kina bidhaa ya mwisho ambayo ndio jawabu la dhumuni la kiwanda lakini ili kupata bidhaa lazima kiwe na hatua za uchakataji wa malighafi ili kuapata bidhaa ya mwisho. Hapa ndio tutakapo rudi kwenye uwekezaji mkubwa wa sekta ya,

i. Kilimo- nilazima tuwe na kilimo chenye tija kwa upana wake ili kuwa na malighafi zitakazo weza kuendana na uhitaji wa viwanda mfano, tuna viwanda vya juisi lakini je tunalighafi za kulisha hivyo viwanda? Mfano leo mtu kaanzisha kiwanda cha juice ya ukwaju, mapera, alovera kuna wakulima wakubwa wa mazao haya na je upatikanaji wake unaendana na mahitaji?ii. Masoko- upatikanaji wa masoko hutegemea vitu vingi lakini vya muhimu mfichuo wa bidhaa kwa walengwa na ubora wa bidhaa. Lakini pia upatikanaji wa malighafi nje na ndani ya nchi lazima kuwe na urahisishaji ambao utapunguza gharama za uendeshaji.

3. Eneo halisi linalo endana za uwekezaji wa aina ya kiwanda - kuna mijadala mingi sana kuhusu eneo la uwekezaji hususani viwanda, je ni bora viwanda viwe karibu na mtumiaji wa bidhaa au miundombinu itakayo wezesha kumfikia mtumiaji wa bidhaa au viwanda viwe karibu na mahali ambako malighafi zinapatikana? Yote haya hutegemea, sera ya serikali kwenye suala la viwanda au stahilimi ya bidhaa ili kufika kwa mlengwa, Mfano bidhaa ya nyama zinazo safirishwa kwenda nchi za nje.

4. Sera ya kitaifa -Si suala la mtu mmoja mmoja kufanya mapinduzi ya viwanda bali serikali ina wajibu wa kuhakikisha inajitoa kwa hali na mali ili kufanya adhma ya viwanda itimie kwa kufanya kila mahtaji la viwanda kimkati yanakua mepesi, nikimaanisha kutenga ardhi na maeneo kwa ajili ya viwanda kwa bei inayo endana na uchumi wa nchi, kupunguza kodi ya uzalishaji wa bidhaa ili kupunguza gharama za bidhaa, kupunguza kodi na tozo zisizo na umuhimu ili kurahisisha viwanda vidogo vidogo kukua, kutoa mikopo kwa viwanda vidogo kwa masharti nafuu hususani wazawa. Kusaidia wajasiriamali kwenye njanja ya viwanda kupata masoko ya ndani serikali na pia nje ya nchi kwa kuwapa kipaumbele.

JE, IWEPO HAJA YA MAWAZIRI KUWANIA NAFASI ZA UWAZIRI?
Hi ingesaidia saana hususani kwenye wizara ya viwanda na biashara na pia mawaziri wapewe malengo ya kufikia kwa kipindi cha mwaka mmoja au miwili. Ni lazima wizara ya viwanda na biashara iwe na kusudi la kutimiza kila mwaka na baada miaka kadhaa ili kufanya masuala ya viwanda nchi kuwa na muendelezo unao ishi. Mfano leo kuna kozi zinatolewa na chuo kikuu cha Mzumbe za masula ya viwanda lakini ukienda wizarani hukuti wale watu wakiwa ndani ya wizara wakileta chachu upande wa viwanda. Hakuna muunganiko kati ya vyuo vinavyo toa kozi za viwanda vyenyewe na wizara husika na hilo ni tatizo.

USHAURI
Tatizo la Ajira nchini si suala litakalo malizika kwa kutoa ajira bali ni suala la kimkakati ambalo litapunguzwa/litamalizwa endapo serikali itawekeza kwenye sekta ya kilimo na pia sekta ya viwanda. Kuwekeza kwenye hizi sekta kutapunguza zaidi ya asilimia 75% ya tatizo la ajira na pia kuikwamua nchi kiuchumi has. Ni muhimu serikali utimie wataalamu wake kubalisha mawazo ya vijana wengi kuamini kilimo ni cha watu masiki na viwanda ni vya watu matajiri.

Ni muhimu kuwapa vijana mitaji na elimu ya kilmo, kuwapa vitendea kazi ili wafanye kilimo biashara na hatimaye kutafuta masoko yenye tija, lakini ni muhimu tuamini tunaweza kuto agiza baadhi ya bidhaa za vyakula kwa kujilimia sisi wenyewe ni muhimu serikali ikae na wamiliki waviwanda ijue mahitaji yao na namna ya kupata majawabu kwa kupitia majawabu ya ndani ya nchi.

Muhimu serikali iweke msisitizo kwa wasomi wa ndani ili wenye kutoa mchango kwenye viwanda.
Kuna haja ya kuiongezea thamani na nguvu SIDO ili iweze kufanya mambo makubwa na muhimu yenye kuleta mapinduzi katika sekta ya viwanda nchini.
 
Back
Top Bottom