Bwana Matunda
New Member
- Jul 16, 2021
- 4
- 5
JE, MAJI WANAYO TUMIA KUMWANGILIZIA NA KUOSHEA MCHICHA UNAOKULA UNAYAJUA?
Siku moja nilipata wasaa wa kutembelea maeneo ya Buguruni-marapa,Dar es salaam katika bonde kubwa ambalo watu wa maeneo ya pale utumia kulima mbogamboga.
Furaha yangu ilifika kiwango cha juu sana baada ya kukutana na watu wa umri tofauti wakiwa katika bustani zao wakiendela na kilimo.
Gafla furaha ikatoweka😔 baada ya kuoneshwa maji yanayotumia kumwagilizia na kuoshea mboga ambazo zipo tayari kwenda sokoni.
Maji yalikuwa ni MACHAFU kupita kiasi,haukuwa mto bali ni mtalo unaopitisha maji toka gereji,majumbani na sehemu nyingine. Soko la Buguruni na mitaa ya karibu na bonde lile ndio sehemu ya maeneo mboga zinapouzwa kila siku.
Usalama wa mbogamboga zinazotoka katika bonde lile ni mdogo sana. Just Imagine umenunua majani ya maboga kwa haraka zako umeosha au hujaosha kwa uhakika ni wadudu au bakteria kiasi gani uwa umewakula kila siku?
Ukweli kuna maeneo(mashamba/bustani) ulima mbogamboga au matunda kwa njia zisizo salama kwa mlaji.
mwisho wake mtu upata magonjwa(kuhara,kipindupindu,maumivu ya tumbo n.k).
UKIENDA SOKONI/GENGENI (LOCAL MARKETS)
Unaweza kuuliza baadhi ya maswali. Muulize mkulima(kama umeenda kwenye masoko ya wakulima) maswali kwa lengo la kujua njia au mbinu alizotumia katika kilimo cha mbogamboga au matunda anayouza.
Wakati mwingine ukipata nafasi mtembelee shambani/bustanimi kwake ujionee shughuli zake anavyo ziendesha.
Kabla hujanunua muulize;
▫️Umetumia aina gani ya mbolea katika mbogamboga hizi unazoziuza?
(Hakikujibu samadi- kinyesi cha wanyama mpe hongera,na akikujibu mbolea za kemikali i.e UREA,CAN n.k mwambie atakupoteza mteja wake).
👉🏽 Kwenye swali la mbolea hakijibu hatumii mbolea aina yeyote,muulize njia gani anatumia mpaka mbogamboga zake zinakua?.
▫️Dawa gani unatumia kuuwa wadudu katika mbogamboga pindi zinapokuwa shambani?
(Akijibu viwatilifu au sumu za kuulia wadudu mwambie atakukosa mteja wake endapo ataendelea kutumia hivyo).
▫️Nani mwingine anazihudumia mbogamboga zinapokuwa shambani/bustanini?
Unajua kwanini unamuuliza maswali haya,ni hivi sio kila kinachoitwa "Local" ni salama.
Ndimi Bwana Matunda