Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Hii ni nikuu kutoka bandiko langu hili Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!
Maneno hayo ni maneno makubwa sana na yenye maana kubwa kwasababu yanahusu "kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao".
Uhuru wa watu kuwachagua viongozi wanaowataka ndio haki ya tatu ndani ya katiba yetu ya 1977. Haki kuu ya kwanza ni haki ya uraia, haki kuu ya pili ni haki ya kuishi, na haki kuu ya tatu ni haki ya kuchagua na kuchaguliwa, ibara ya 5 na ibara ya 21.
Haki hii ina sherti moja tuu la umri wa miaka 18 kupiga kura, umri wa miaka 21, kuchaguliwa diwani au mbunge, na miaka 40, kuchaguliwa kuwa rais wa JMT.
Hakuna shurti la kulazimishwa kuwa mwanachama wa chama cha siasa, kilichofanyika kuchomekea shurti la mgombea kudhaminiwa na chama cha siasa, ndani ya Katiba yetu ni uhuni na ubatili tuu uliofanyika kiubatili kinyume cha katiba yetu na Mahakama Kuu iliisha ubatilisha ubatili huo!.
Kiongozi yoyote anapoandika ama anapohutubia, kuna mambo mawili, kwenye andiko lake ama hotuba yake.
1. Kati ya andiko la Kiongozi kuna vitu ni maono, mawazo, maneno na maandishi ya Kiongozi yeye mwenyewe kutoka moyoni mwake, kichwani mwake, mawazoni mwake, yaani ni yeye mwenyewe halisi.
2. Viongozi wana wasaidizi ambao huwa wanawaandikia talking notes, na kwa rais wa nchi, ana wasaidizi hotuba ambao wanamuandalia nini cha kusema kwa kumuandikia, kisha Rais kwanza anapitia kile alichoandikiwa lakini sio chake, anaweza kuongeza chake au kupunguza, na ndipo anakuja kuhutubia au kutoa andiko.
Wakati akihutubia, sisi tunaosikiliza, tukisikia kila Rais anachosema kwenye hotuba yake, tunahesabu kila kilichosemwa ni rais kusema.
Wakati Rais akihutubia, kila anachosema ni Rais kusema, huwezi kujua kipi ni cha kwake na kipi ni ameandikiwa tuu lakini sii cha kwake.
Hii pia hutokea kwa wasomaji wa habari kwenye TV zote na redio zote, watazamaji na wasikilizaji, wanamuona mtangazaji, wanamsikiliza mtangazaji, wao wanajua hizo habari wametangaziwa na mtangazaji fulani, wao wanajua ni mtangazaji huyo ndie anajua habari hizo, kumbe hawajui kazi ya mtangazaji wa habari ni kutangaza tuu habari alizoandikiwa na wengine, yeye kazi yake ni kusoma tuu!.
Vivyo hivyo kwenye hotuba za Viongozi, kuna Viongozi wanasoma tuu hotuba walizoandikiwa na wengine lakini sio mawazo yao, sio maneno yao, ila ni matamshi yao!.
Kama nolivyosema kwenye habari, mtangazaji unaandikiwa ,kisha unapewa kuipitia habari hiyo , kwa RTD, taarifa ya habari ni dakika 10, mtangazaji unatakiwa kuipitia nusu saa kabla, ili uielewe na unaposoma, una soma kitu unachokijua.
kitendo cha kuichukua habari ambayo hujaiandika wewe, ukaipitia na kuisoma as if ni umeiandika wewe, kinaitwa "presence", ndio maana watangazaji huitwa presenters, kazi yao ni ku present tuu.
Kuna wakati msomaji wa habari unapitia habari usiyoielewa, unapaswa uulize, ili usisome kitu usichokielewa, ili ukisoma ile presence iwepo. Lakini katika mitikasi hii na ile, kuna siku unakuwa umechelewa kupitia news kabla, hivyo unasoma tuu kwa uzoefu, hata ukikutana na kitu usichokielewa, unakisoma tuu hivyo hivyo, na wasikilizaji na watazamaji watasikia tuu nabkuelewa, lakini kwa watu sensitive na kitu kinachoitwa graphology, utamnote mtangazaji ana fanya stammering, then unajua huyu hajapitia, hivyo anasoma kitu asichokijua, anasema kitu alichoandikiwa lakini hakijui.
Vivyo hivyo hutokea kwenye hotuba za Viongozi anaandikiwa kitu asichokijua, anapitia hotuba, kisha anahutubia kitu asichokijua, hii inaitwa "paying lip services".
Maneno hayo ya Rais Samia kwenye andiko lake ni maneno makubwa, mazito Bonafide Genuine, kwenye bandiko hili, nikasema "Rais Samia atabarikiwa sana kama atatekeleza hili"
Sasa sheria mpya ya uchaguzi imeishatungwa, its very unfortunately sheria hiyo mpya bado ina ubatili ule ule tunaoupigia kelele, hali inayonifanya kuanza kujiuliza, hivi maneno haya "Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi, yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza”
Jee ni maneno ya Rais Samia mwenyewe au aliandikiwa?!. Jee hii sheria mpya ya uchaguzi, yenye ubatili ule ule, italeta vipi ushindani wa haki wakati Rais Samia ameahidi, "kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza”
wakati sheria mpya ya uchaguzi, watu bado hawana haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka, bali Watanzania tunalazimishwa kuwachagua viongozi waliopitishwa na vyama vya siasa na sio viongozi wanaowataka!.
Watanzania walitaka sheria mpya ya uchaguzi yenye kumpa haki Mtanzania,kumchagua kiongozi anayemtaka,na kila Mtanzania kuwa huru kugombea na kuchaguliwa。 Sheria tulioletewa ni sheria ile ile batili,inayokwenda kinyume cha katiba ya JMT,hivyo hapa tumepigwa lip services!
Watanzania walitaka Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi,kilichofanyika ni wame wabadilishia tuu jina la Tume ya Uchaguzi kutoka kuitwa Tume ya Uchaguzi, NEC, kuwa Tume Huru ya Uchaguzi,INEC,lakini tume ni ile ile,watu ni wale wale!,this is paying lip services!。
Bado tunaomba Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025,na sheria mpya ya uchaguzi yenye uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa!。Ili haya yafanyike ni lazima kufanyike minimum reforms kwenye katiba yetu,muda upo na unaruhusu,kinachatakiwa ni utashi wa kisiasa na sio to pay lip services!。
Tafsiri ya alichokisema Rais Samia, na kilicholetwa kwenye sheria mpya ya uchaguzi ni sawa na kusema, jee kuna uwezekano Rais Samia na yeye is just paying 💋 services kwenye baadhi ya kauli zake na ahadi zake?.
Paskali

hii ni nukuu ya Rais Samia katika andiko lake la miaka 30 ya Vyama Vingi nchini Tanzania. Naomba nifanye revisiting ya bandiko hili la Julai 2, 2022."Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi, yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza” - Samia Suluhu Hassan Mwisho wa kunukuu.

Last edited: