Uchaguzi 2020 Je, kuna uwezekano kutangaza nia kugombea Urais kupitia CHADEMA kwa baadhi, kunatumika kama kichaka cha kujifichia aibu ya kushindwa ubunge?.

Acha upotoshaji wa kijinga Paskali, kwani ukitia nia ya kugombea urais ndio huwezi kugombea ubunge? Akina Kigwangalla, Makamba, Mwigulu nk wote hao walijitokeza kugombea urais wa ccm, mbona wote ni wabunge hivi sasa?
Nafikiri mtoa mada yupo sawa kabisa. Wengi wanatia nia wakijua hawana sifa za kuwa Marais na hata chembe ya kupamba na JPM hawana kwa hiyo ni kama kuondoa aibu kwenye jamii wanajionyesha kuwa nao eti bado wanakubalika. Lakini ukweli ni kuwa Chadema na hao wote waliotia nia hamna kitu bora wangekaa kimya.
 

JPM angekuwa anaamini kweli anaweza kushinda kihalali asingenajisi box la kura.
 
Fafanua kulinajisi box la kura kivipi?

Kuagiza makundi ya green guards kuwapiga wapinzani hadi kuwaachia vilema, na hata vifo ili ccm ipate ushindi. Kutumia vyombo vya dola na tume ya uchaguzi, kusimamia hujuma na wizi wa mabox ya kura kwa faida vya ccm. Kuwaagiza wasimamizi wa uchaguzi kukimbia kupokea fomu za wagombea wa upinzani. Kutangaza matokeo yasiyo halali, kisha vyombo vya dola kutumika kuzima hasira za wananchi wasiokubali kuhujumiwa.
 
Ina maana hata jumuia za kimataifa huwa hazioni huu uchafu? Maana kila uchaguzi huwa wanasema ulikuwa huru na hauna matatizo.
Hao green guard huwa wanaingia kwenye vituo vya kupigia kura? Maana sare za vyama huwa zinazuiwa.
Vyombo vya dola huwa vinawashikia wananchi bunduki?
 
pia inawezekana CDM wanataka kuonyesha kuwa wako serious kushiriki uchaguzi halafu watakapotangaza kususia waaminishe watu kuwa ni kweli wamechoshwa na hali ilivyo ndio maana wanasusia uchaguzi ambao walijipanga kushiriki.
 

Jumuiya na kimataifa ukiacha nchi Afrika wote huwa wanaweka wazi kuwa chaguzi zetu sio huru na haki.

Kituo cha kupiga kura kina nini wakati yanaletwa mabox ya kura na green guard, yenye kura za ccm kwa uratibu wa vyombo vya dola?

Vyombo vya dola huwa vinasimamia kutangazwa matokeo ya kura yasiyo na ridhaa ya wananchi.
 
Kubalini tu Ccm chini ya JPM imefanya kazi kubwa sana. Na inakubalika hayo mengine ni visingizio tu.
 
!
!
Ushindi ni lazima. Tume yao, Polisi wao, Wakurugenzi ambao ni wasimamizi wao ukijumlisha na mikwara ya jiwe kuhusu kumtangaza mpinzani unafikiri kuna nini hapo
 
Taarifa nilizonazo ni kwamba mchungaji Msigwa amekataa kumuunga mkono Nyalandu kama walivyokubaliana awali hali iliyopelekea Mbowe atie nia ili kuja na plan B.

Inadaiwa mchungaji Msigwa ni pandikizi lenye nguvu za " ghafla"

Maendeleo hayana vyama!
Kwa mbaaaali ni kama nakuelewa vile!!! Embu, tuupe muda utasema
 
Utopianism
 
Kwani unafikiri hajui hilo? Anajua sana ila shida yake ni kuwadhalilisha watu ili kumpendezeaha Msukuma mwenzetu.
 
Kuna waandishi wengine wasen-e tu kama was-nge wengine. Halafu mtu kama huyu anaitwa mwandishi. Ataandika nini badala ya ufala wa njaa alioujaza kichwani.
 
Uzi wa Leo uko chini ya kiwango ngoja Tu nipite hivi
 

Pia ni mbinu ya kulazimisha kutoguswa, niguse unuke. Mfano Freeman Mbowe kuna uwezekano akatuhumiwa na ubadhirifu ndani ya chama chake Mbowe anatumia kugombea kama fursa ya kujinasua ikitokea kuna potential tuhuma dhidi yake atalazimisha uteuzi ili akikamatwa au akipelekwa mahakamani basi ionekane anakamatwa kisiasa na sababu ikiwa kugombea urais.

Msigwa yeye anatumia kugombea urais kama njia ya kurahisisha kugombea ubunge. Atajwe tajwe mara nyingi, asikike mara nyingi kwani hali ni ngumu kiubunge kwa upande wake, hivyo kuliko atumie kiinua mgongo chake kwa kampeni ni bora atumie kiki ya urais kumpaisha.

Nyalandu yeye lengo lake ni kujiimarisha kibiashara na uhusiano wake wa nje na marafiki zake wa nje. Ndoto yake kubwa ni kugombea urais seriously 2025.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…