Je, kunaweza kuwa na wasimamizi watatu wa mirathi?

GITWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
1,572
Reaction score
1,781
Poleni na majukumu wanasheria.

Napenda kujua iwapo sheria inaruhusu wasimamizi zaidi ya mmoja wa mirathi yaani kama watatu hivi.

Maana kuna familia ina watoto wa mama watatu tofauti na wako kwenye mchakato wa mirathi lakini suala la mtu mmoja kupewa usimamizi wa mirathi linawachanganya.

Wao wanataka kila mzaliwa wa mama mmoja awe katika usimamizi wa mirathi.

Natanguliza shukurani kwenu wanasheria wasomi kwani maoni yenu yatakuwa ufumbuzi wa hii sintofahamu.
 
Kuna uhitaji wa maoni upande huu wakuu
 
Hiyo ndio tabu kuzaa kama panya tena na wanawake tofauti..
 
Mwaliko wa wanasheria wasomi huu.

Mbona mmejifungia ndani?
 
Nawasubiri maana hii ni sensitive issue
 
Poleni na majukumu wanasheria.

Napenda kujua iwapo sheria inaruhusu wasimamizi zaidi ya mmoja wa mirathi yaani kama watatu hivi.

Maana kuna familia ina watoto wa mama watatu tofauti na wako kwenye mchakato wa mirathi lakini suala la mtu mmoja kupewa usimamizi wa mirathi linawachanganya.

Wao wanataka kila mzaliwa wa mama mmoja awe katika usimamizi wa mirathi.

Natanguliza shukurani kwenu wanasheria wasomi kwani maoni yenu yatakuwa ufumbuzi wa hii sintofahamu.
inawezekana kuwa na msimamizi zaidi ya mmoja.

Hivyo wote watatu wanaweza kuwa wasimamizi wa mirathi ikiwa watapendekezwa na familia na mahakama ikawateua. Sheria ya usimamizi wa mirathi inaruhusu.

Hapo ninachokiona nikukosekana kwa uelewa juu ya hasa nini maana ya usimamizi wa mirathi.

msimamizi wa mirathi anasimamia makubaliano yaliyofanywa na familia, Hana mamlaka yakubadili makubaliano hayo na utekelezaji wake unasimamiwa na mahakama.
 
Asante kwa andiko lako mkuu, naendelea kupokea maoni.
 
Alipie Kwanza,asitake kutumia elimu yetu bure, wenyewe tumeilipia huko law school!!
Wote wakiwa kama wewe fukara wote hawata pata na haki.

"Kuna wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna"
 
Back
Top Bottom