Mkuu, kuoa ni kupata na kupoteza! Unapata mke/mme, mwenzi wa maisha, rafiki wa karibu, na mtu wa kufarijiana, kuombeana, kusaidiana naye siku kwa siku.
Kuoa ni kupoteza pia. Kama unataka ndoa iwe ya furaha kati yenu, ni lazima ukubali kupoteza. Moja ya vitu unavyopoteza ni uhuru. Kama kuna vitu ulizoea kufanya kabla ya kuoa lkn mwenzio havipendi lazima ukubali kuvipoteza. Eg. Km ulikuwa unahang out na friends (male or female) mpaka usiku wa manane lkn mwenzio hapendi, itakubidi ubadilike ili usije ukaiweka rehani ndoa yenu.
Huwezi kuoa na ukaendelea kuwa na kiwango hicho hicho cha uhuru, lazima ukubali kupoteza kwa manufaa ya ndoa.