Write your reply...sioni haja ya kupaki gari kwa mda wote huo . automatically lazima kuwe na madhara
Hata hivyo hadi member mwenzetu anauliza hivyo atakuwa na sababu za msingi. These are few tips kama itamlazimu.
A. Ipaki gari yako lakini unashauriwa " kupiga misele" walau mara moja kila wiki mbili, kuanzia walau km 30 tena kwa spidi zaidi ya 50kph ili kuifanya engine iendelee kuwa hai. Kupiga less kila siku haisaidii kwasababu baadhi ya sehemu kama valves, transmission n.k haziwi engaged kikamilifu
B. Kama utakuwa mbali nz hilo haliwezekani fanya yafuatayo
1. Jaza mafuta "full tank" ili ulinde kutu zisiingie kwenye tenk
2. Inyanyue gari kwa " four jacks" kuzuia tairi kuharibika. Zisiguse chini. Usi engage hand brake bali iache gari free ili kulinda breki pads
3. Hifadhi gari lako gereji ya ndani ikiwezekana funika na cover lake ili kuzuia kutu
4. Mwaga oil na tia oil safi, fungua plugs zote kisha tia oil kiasi ili ikae juu ya pistons kuzuia kutu kisha funga hizo plugs, japo hii italeta moshi kiasi baafaye utakapowasha gari lako
5. Fungua + terminal ya battery yako ili kuizuia isipoteze nguvu. Paka grisi kwenye maungio ya battery kuzuia kutu
Kumbuka kuondoa uchafu ndani ya gari unaoweza kuwavutia panya na wadudu wengine
Hata hivyo, fanya haya pale tu unapolazimika kuipaki gari, maana uharibifu mwingine hauzuiliki. Wengine warahazua