Mara nyingi huwa ni tatizo la kisaikolojia(afya ya akili)
Kuna levels mbalimbali za tatizo hilo, kuna wengine inaweza isionekane madhara yake moja kwa moja kwasababu maisha yao yanakwenda fresh na hana matatizo na mtu
Kiasili binadamu ni social animal yaani maisha yetu ni maisha ya kujumuika na tegemezi kwa wengine
Mtu anayependa kuwa peke yake muda wote anakua na tatizo la kisaikolojia
Mara nyingi sana anakua HAJIAMINI anajihisi hayupo SAWA anajihisi Tofauti au anajiina ANAUDHAIFU fulani na anaogopa hicho anacho hisi kinaudhaifu kitawakwaza au kitajulikana na wengine.
Lakini pia fear of rejection nayo ni shida kubwa inayo wakabili watu wapweke
Yaani anaona akitongoza, akitaka urafiki na mtu, akijieleza, akiomba kitu ATAELEWEKA NA KUKUBALIKA?
Kuepuka hayo anaamua kua mpweke
Kuna sababu nyingi ila kimsingi ni tatizo la Afya ya akili