LGE2024 Je, kura ya hapana kwa Mgombea wa Mtaa/kijiji inaweza kuwasaidia Vyama vya Upinzani?

LGE2024 Je, kura ya hapana kwa Mgombea wa Mtaa/kijiji inaweza kuwasaidia Vyama vya Upinzani?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Kanuni ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu inasema kuwa hapatakuwa na mgombea kupita bila kupingwa na hivyo itabidi apigiwe kura ya hapana au ndiyo.

Leo nimemuona Tundu Lissu akiwafundisha wapiga kura wa Nyamongo - Tarime kuwa siku ya uchaguzi wampigie mwenyekiti zliyepita bila mpinzani kura ya hapana kutokana na mgombea wao wa CHADEMA alienguliwa pasipo sababu yeyote.

Soma Pia: Uchaguzi Serikali za Mitaa 2024: Hakuna kupita bila kupingwa, atakapopatikana mgombea mmoja, atapigiwa kura za ndiyo au hapana

Je nani atahesabu hizo kura za ndiyo na hapana. Je utaratibu huu utasaidia?.
 
Wakala wa kura ya HAPANA atakuwa nani?
 
Kura za Upinzani huwa zinapigwa kwenye social media mitaani huwa wanapiga wana CCM , mimi mwenyewe sina muda wa kupanga ma foleni
 
Kwa uhalali kura za hapana zitashinda kura za ndiyo,mwisho wa kufungua sanduku la kura zote zitabadilika na kuwa kura za ndiyo.
 
Back
Top Bottom