Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Mzee wetu Ysufu Makamba, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM alitoa kauli yenye ukakasi mkubwa Sana kwenye Mkutano Mkuu uliopita, kuwa eti viongozi wema huwa hawafi na akatolea mfano wa JK na Kinana, kuwa Bado wako hai hadi Leo, Kwa kuwa wamewatendea mema watanzania!
Ingawa kauli hiyo Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan alijaribu kuisahihisha Kwa kusema kuwa Mzee wetu Makamba alikuwa ameteleza ulimi Kwa kuyatamka maneno hayo.
Ni nahau nzito Sana na inabidi uitafakari Kwa makini Sana, Ili ujue Mzee wetu Makamba alimaanisha Nini katika kuyasema hayo maneno?
Hata hivyo Kwa kufanya tafsiri yangu ya namna nilivyoyaelewa maneno hayo ya vijembe, ni kuwa hata ule msiba mzito tulioupata kama Taifa mwaka Jana, ulitokana na "maamuzi" ya Mungu ya kutuondolea kiongozi wetu, kutokana na "maovu" yake mengi Sana, aliyowafanyia watanzania, hususani wapinzani wa nchi hii.
Nimesema kuwa maneno hayo yanaweza kuwa ni ukombozi Kwa Taifa letu.
Watu wengine wanaweza kuniuliza ni Kwa vipi maneno hayo yanaweza kuwa ni ukombozi Kwa Taifa letu?
Jibu ni rahisi tu, Kwa "nature" ya kibinafamu ni kuwa ingawa kifo tumeumbiwa sisi binadamu, hata vitabu vya dini zetu vinabainisha hayo.
Kwa mujibu wa maandiko kwenye Biblia yanasema, tuliumbwa Kwa mavumbi na tutarudi Kwa mavumbi na kwenye Quaran imeandikwa kuwa Kila nafsi itaonja umauti.
Kwa hiyo katika dini zote zimebainisha kuwa ni LAZIMA itafika siku sisi binadamu tutakufa.
Hata hivyo Kwa "nature" ya binadamu yeyote, anakiogopa kifo, Kwa hiyo Kwa "kuwakumbusha" viongozi wetu kuwa, watu wema ndiyo wenye maisha marefu hapa Duniani, kutawafanya viongozi wanaotutawala watende mambo mema na watende haki, wakati wa utawala wao, Ili waweze kuishi maisha marefu zaidi.
Kwa watawala wetu kututendea mambo mema watanzania, kama vile kuwa na utawala Bora, unaozingatia Sheria, kuzingatia usawa katika utawala wao, na siyo kuvinyanyasa vyama vya upinzani wakati vinatekeleza wajibu wao Kwa mujibu wa Sheria za nchi hii na kuepuka kufanya ufisadi, ndiko kunakoweza kuwa mwanzo wa kulikomboa Taifa letu.
Hongera Mzee Makamba Kwa kuyatamka hayo maneno hadharani
Mungu ibariki Tanzania