Je kusudi la Mungu kumuunba mwanadamu ilikuwa ni lipi kati ya haya mawili?

Nikae pembeni kwa kumuogopa nani?

Wewe usiyeweza kujibu swali ndiye wa kukaa pembeni.

Huna ubavu wa kunifanya mimi nikae pembeni.
Noted ... but uwage unakuja basi kwenye mada za kisayansi pia.. huwa tunahitaji mchango wako pia
 
Mungu ametuumba ili tumuabudu katuwekea ardhi yenye rutuba na Mito inayotiririka maji kwa ajili ya kunywa, wake kwa waume ili tuburudishane na tuzaane. Ametuletea mitume ili itufunze ni nini anachokihitaji tufanye na tufuate ktk kumuabudu.
 
Mkuu hayo majibu yako ni ya kielimu au umetumia akili yako?
 
Mkuu hayo majibu yako ni ya kielimu au umetumia akili yako?
Huo ni mtazamo wangu binafsi baada ya kuona vyanzo vyote vinavyomuelezea Mungu havinipi jibu ambalo linakidhi uhalisia ninaouhisi.
 
Huo ni mtazamo wangu binafsi baada ya kuona vyanzo vyote vinavyomuelezea Mungu havinipi jibu ambalo linakidhi uhalisia ninaouhisi.
Maadamu umesema ulichokijibu ni mtazamo wako tu na si kielimu basi na mie hebu nitumie mtazamo wangu kuona kama kweli jibu lako lina uhalisia.

Umesema hakuna anayejua lengo la Mungu kutuumba sisi lakini hapo hapo unatuambia tuishi tu,hauoni kwamba huko kusema sisi tuishi tu ni sawa na kusema kuwa lengo la Mungu kutuumba ni kuja kuishi tu vile tujisikiavyo?

Kwa sababu hili swali la kutaka kujua kwanini Mungu katuumba hatuwezi kulipotezea na sidhani kama Mungu anaweza akalifanya jambo kubwa kama hili kuwa siri kiasi kwamba hadi watu watumie mitazamo yao binafsi.

Kwa sababu vp ikiwa lengo la Mungu kutuumba ni tofauti kabisa na sie tunavyoishi,je hiyo italeta maana gani?maana hatujui kwanini ametuumba na hivyo hatuwezi kusema sie tuishi tu kwa sababu hatujui lengo lake.
 
Binadamu yupo duniani kwa ajili ya kufanya kazi...

Mengine yapo kwa ajili ya kuwajaza hofu binadamu ili tusidhuriane...


Cc: mahondaw
 
Noted ... but uwage unakuja basi kwenye mada za kisayansi pia.. huwa tunahitaji mchango wako pia
Kuna vitu viwili sijawahi kuvipotezea hapa JF.

Mtu anayenitaja (tag) na mtu anayeninukuu.

Yani hata kama kuja kuuliza tu "hapa nini kinaendelea?" nitakuja.

Au hata kuna swali naulizwa sijui jibu nitasema tu sijui.

Kwa hiyo ukiona thread nzuri ni tag tu nitakuja.Unajua hapa threads nyingi halafu mimi mostly nangalia zile ambazo nimo tayari (watu ninaojibizana nao) na zilizo juu kwa kujibiwa sana.
 
ahahahahhahahah kweli kabisa wasikimbie maswali kwa mbinu za kitoto
 
Mungu ametuweka duniani ili tumjue, tumpende, tumtumikie na mwisho turudi kwake mbinguni
 
Watafute Mashahidi wa Yehova watakupa jibu zuri. Wapo vizuri sana kwenye kuchambua biblia. Wasearch hata google wapo.
 
Aliumba binadamu ili afanye kazi kwa kutumia utashi na sio kumwabudu kwani anajua kila kitu afanyacho binadamu. Huenda kumwabudu ni kujipendekeza . Ni kuchapa tu kazi huku ukijua jema na baya .Siku za mwisho utaulizwa aliyekuambia uniabudu ni nani? Kwa wakristu swali la nyongeza kutoka kwake " Sina mtoto niliyemtoa kafara ili kumkomboa binadamu kwani sibishani na shetani" Utajibu nini? Kulia na kusaga meno.
 
Watafute Mashahidi wa Yehova watakupa jibu zuri. Wapo vizuri sana kwenye kuchambua biblia. Wasearch hata google wapo.
hahahaha. Shida ya wale jamaa ukisha tu wakaribisha siku moja watakupigia hodi kila siku kama vile mtu hana kazi ya kufanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…