Tohara ya Wanaume.Baada ya upasuaji.
Tohara ya kiutamaduni
Katika ma
kabila mengi ya
Afrika mvulana anatahiriwa ili kuingizwa katika kundi la
wanaume wanaopaswa kuwajibika katika
jamii.
Desturi hiyohiyo inaonekana pia kati ya watu wa
Pasifiki k.mf. Wapolinesia wa
Samoa,
Tonga na
Niue, vilevile kati ya Wamelanesia wa
Fiji na
Vanuatu.
Wakazi asilia wa Australia huwa pia na tohara ya wavulana.
Tohara kama amri ya kidini
Uyahudi
Kwa
Wayahudi tohara ni ishara ya
agano lao na
Mungu na inapaswa kufanyika siku ya nane baada ya
mtoto wa kiume kuzaliwa ili kumwingiza mapema katika
taifa la Mungu.
Kufuatana na habari za
Biblia Ibrahimu alikuwa mtu wa kwanza aliyepokea amri ya kutahiriwa kama alama ya agano (
Mwanzo 17).
Ukristo
Yesu mwenyewe alitahiriwa siku ya nane kama Wayahudi wote wa kiume. Tohara ya Yesu inakumbukwa kwa sikukuu maalumu katika makanisa mengi duniani hasa
Waorthodoksi.
Agano Jipya inaonyesha jinsi gani suala la tohara lilikuwa motomoto mwanzoni mwa
Kanisa, wakati Wakristo wengi walitoka katika Uyahudi.
Kufuatana na kitabu cha
Matendo ya Mitume (15:23-29)
Mtaguso wa Mitume uliofanyika
Yerusalemu uliamua Wakristo kutoka mataifa wasilazimishwe kutahiriwa.
Hasa
Mtume Paulo alisisitiza kwamba jambo hilo si muhimu tena, cha maana ni kuwa watu wapya kwa imani.
"Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya" (
Gal 6:15).
"Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili" (
Fil 3:3).
Hata hivyo Wakopti wa Misri na
Ethiopia wameendelea kutahiri watoto wao.
[
Uislamu
Katika
Uislamu tohara hufundishwa kama wajibu wa kidini kwa kila mwanaume.
Hakuna amri katika
Kurani kuhusu tohara lakini inatazamiwa kama sunna ya
mtume Muhamad. Kwa imani hiyo ni ishara ya mitume ya kwamba walizaliwa bila govi katika hali ya kutahiriwa tayari.
Utekelezaji wa tohara huwa ni tofauti kati ya nchi na nchi; mara nyingi mtoto mdogo hutahiriwa kwa umri kati ya miaka 5 hadi 10. Katika mazingira ya mjini wazazi wanawahi siku hizi kutahiri mapema.
Tohara kama hatua ya kiafya

Muda mrefu sana na nyembamba govi inaweza kuwa dalili za tohara matibabu
Siku hizi hata ma
taifa yasiyokuwa na
desturi hiyo yanaanza kuijali kwa sababu za
usafi na
afya.
Ni kwamba tohara inapunguza hatari ya mtoto kupatwa na
fimosis.
Imethibitishwa kuwa inapunguza uwezekano wa kuambukizwa
ukimwi pamoja na hatari ya magonjwa mengine kama
kansa ya uume.
Katika nchi kadhaa sehemu kubwa ya watoto wa kiume wanatahiriwa mara baada ya kuzaliwa kwa sababu hizi za kiganga. Kwa mfano,
huko Marekani asilimia 56 za wavulana wote waliozaliwa mwaka 2005 walitahiriwa katika hospitali walikozaliwa. Hata hivyo katika nchi
hiyo kuna kampeni dhidi ya tohara kutokana na hoja ya kwamba mara nyingine upasuaji hauendi vizuri na kusababisha madhara ya kudumu kwa viungo vya uzazi.