Je, kuwa na website tu kunatosha kuanzisha biashara?

Je, kuwa na website tu kunatosha kuanzisha biashara?

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Hili ni swali ambalo huwa nakutana nalo mara kwa mara ninapokuwa katika shughuli zangu hasa pale ninapomsaidia mtu kuanzisha biashara. Mara nyingi wanaouliza swali hili ama huwa wanataka kujifunza au basi wanakuwa wanaona kama haina umuhimu.

Katika kuwashauri huwa nawaambia kwamba Unapofikiria kuanzisha biashara yoyote ile hata kama ni ya kuuza karanga basi anza na "website"Kuwa na website ni hatua ya kwanza na ya muhimu ya kufanya branding ya biashara yako. Kuwa na website kuna kuwezesha kuwasiliana na wateja wako.Kuwa na website kunawezesha wewe kuiweka idea yako katika maandisha na kuwa na malengo. Kuwa na website kuna kusaidia kubadilisha mtazamo wako kuhusu biashara yako, badala ya kuichukulia kuwa ni biashara ndogo unaiona kuwa sasa ni biashara kubwa ambayo ina uwezo wa kufikia dunia.

Kwa kawaida watu hawaelewi. Kwa mfano, kama wewe unafanya biashara ya duka la nafaka au genge la mboga mboga unaweza kujikuta unapata fursa ya kupeleka bidhaa zako nje ya nchi just kwa sababu kuna mtu katika pita pita yake amekuta taarifa zako mtandaoni. Baada ya kuziona anakutafuta na ghafla unajikuta una dili ya kupeleka maparachichi Uholanzi.

Binafsi naamini kwamba ni nauu zaidi kufungua website kuliko kukodisha fremu ya biashara hivyo basi ni vyema tukapeana hamasa ile wote tuelewe kwamba dunia inabadilika na kwamba unapofikiria kuanzisha biashara basi anza kwa kuiweka online. Ukishaiweka ukaongeza na social media unaweza kufanya market research, ukawasiliana na wateja prospects na hata ukapata wateja kabla ya kuanza production.

Tufanye uchumi wetu uwe na ushindani wa kidunia kwa kuweka mawazo yetu mtandaoni.

Karibu tujadili namna ambavyo tunaweza kupeleka biashara zetu mtandaoni pamoja na faida zake.

Karibuni
 
Sasa bro mimi nikiwa na wazo langu la kuuza karanga za rejareja (mfano) natengeneza vipi website ili kuendana na ilo wazo? Me naona web ni kwa wenye mitaji mikubwa bro maana atakuwa na vitu vyingi vya kufanya kutokana na mtaji. Sasa unakuta mfano mimi nina mtaji wa laki tano je, nitagawa vipi iyo 500k niweze kuendesha web na pia biashara iendelee? Pia ni wazo zuri sana nitalifanyia kazi mkuu.
 
Mkuu.ukiitazama biashara yako karanga kama biashara ndogo hutaona haja ya website ili ukiitazama kama biashara kubwa utaona umuhimu.Kwa kifupi ni lazima uwe na maono makubwa kuhusu biashara yako kabla ya kuchukua hatua yoyote.
 
Mkuu thamani ya biashara itabaki palepale, me naongelea mtaji kama una mtaji mdogo mbao huwezi hata kuafford kuendesha iyo web utaweza vipi kuendesha iyo biashara mkuu?
 
Mkuu thamani ya biashara itabaki palepale, me naongelea mtaji kama una mtaji mdogo mbao huwezi hata kuafford kuendesha iyo web utaweza vipi kuendesha iyo biashara mkuu?
Mkuu,website ni namna bora ya kufikia wateja wengi kwa gharama nafuu.Kwa kutumia website unakuwa na uwezo wa kufikia wateja wengi zaidi.Swali ni je biashara yako imelenga wateja gani?Je mtaji wako ni kiasi gani?Hayo ni maswali ambayo unapaswa kuyatazama kwa umakini katika hatua za mwanzo kabisa na majibu yake yatakupa mwongozo wa nini ni kipaumbele cha biashara yako
 
Back
Top Bottom