Hehehee!! Yaani Raila kakamata map.umbu ya nchi yote, hakuna mwenye uwezo wowote juu yake, inabidi aachiwe afanye atakalo wakati autakao siku aitakayo.
Tatizo hamna jinsi Uhuru anaweza kukabiliana naye bila kujikuta ICC kwa mara ya pili, maana leo akimkamata Odinga kwa haya anaayoyafanya, wafuasi wake watajitokeza kichizi na kufanya vituko vitakavyopelekea wao kuuawa na polisi, maana kama vile kuvamia vituo vya polisi, hapo itakua ni tiketi ya kumrudisha Uhuru kule the Hague.
Hivyo inabidi Raila aachiwe abwatuke na mikwara na kufanya anachohisi kwa muda anaoutaka, labda njia ya kumthibiti ni kuwakamata washirika wake na wafadhili wake kama hao akina Wanjigi, lakini yeye kama yeye ni untouchable, unamgusa tu na nchi inawaka.
Mnamo mwaka wa 1982 alisababisha umwagikaji wa damu mkubwa kuwahi kutokea Kenya, lakini taratibu yote yaliswekwa chini ya mkeka hadi leo kimya.