Je, kuzuia Uchaguzi siyo Uhaini?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Nchini Kenya Raila Odinga ameapa kuzuia Uchaguzi ambao upo Kikatiba nahisi, sasa Je ana uwezo huwo? Na anazuia yeye kama nani? Na Sheria za Kenya zinasemaje juu ya hili la kumzuia Raia asipige kura?
 
Hehehee!! Yaani Raila kakamata map.umbu ya nchi yote, hakuna mwenye uwezo wowote juu yake, inabidi aachiwe afanye atakalo wakati autakao siku aitakayo.
Tatizo hamna jinsi Uhuru anaweza kukabiliana naye bila kujikuta ICC kwa mara ya pili, maana leo akimkamata Odinga kwa haya anaayoyafanya, wafuasi wake watajitokeza kichizi na kufanya vituko vitakavyopelekea wao kuuawa na polisi, maana kama vile kuvamia vituo vya polisi, hapo itakua ni tiketi ya kumrudisha Uhuru kule the Hague.

Hivyo inabidi Raila aachiwe abwatuke na mikwara na kufanya anachohisi kwa muda anaoutaka, labda njia ya kumthibiti ni kuwakamata washirika wake na wafadhili wake kama hao akina Wanjigi, lakini yeye kama yeye ni untouchable, unamgusa tu na nchi inawaka.
Mnamo mwaka wa 1982 alisababisha umwagikaji wa damu mkubwa kuwahi kutokea Kenya, lakini taratibu yote yaliswekwa chini ya mkeka hadi leo kimya.
 
Kenya jengeni ukuta sasa maana mlishindwa kuziba ufa.Uncle Magu kaza buti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…