Eneo ninaloishi kuna vibaka wengi sana. Usiku wanaruka ukluta na kuingia uani mwangu na kuondoka na chochote wanachokikuta iwe ni kikombe, ndoo, beseni, nguo nk. Kuna nondo za ujenzi nimenunua na nataka kuzihifadhi uani. Kwa kuhofia udokozi wa vibaka, nataka niunganishe umeme kwenye hizo nondo ili mshenzi yeyote mwenye nia ya kuzidokoa anaswe au kushtuliwa na umeme.
Je, endapo kweli baada ya kuunganisha umeme kwenye nondo kibaka akanasa na kufa, nitakuwa hatiani?
Naomba jibu zuri linalozingatia sheria za nchi hii.