Je kwa kosa hili NI SAHIHI KWA MKE KUMUITA MUMEWE MJINGA?

swala hili mbona rahisi sana kujua aliyefanya kosa kati ya hawa wawili. je, mtoa mada wewe unadhani kitendo alichofanya huyo mwanamume ni sawa au ujinga?
 
hapa kila mmoja ana makosa yake ila kwa haraka lazima tutamhukumu mmoja ..

.- inaonyesha wakati marehemu yupo inawezekana huyu mwanamke hakuwa karibu sana na hii familia hivyo hata baada ya msiba mwanamke mwenzake bado hakuwa karibu na mjane ndo maana ..
- ushirikiano uliopo kati ya mjane na mwanaume unaonekana umejengeka hata kabla ya kifo cha jamaa
- huyu bwana pamoja na mkewe inaonekana hawana ukaribu sana wakiwa pamoja
- jamaa kutomwambia mkewe juu ya sherehe inatoka na kutokuwa karibu na hiyo familia hivyo alijua tayari itakuwa kikwazo kaika ushiriki
- mwanamke kumwambia jamaa ni mjinga hakufanya jambo la kistaarabu hata kama mme au mke ana matatizo si vyema kutumia matusi katika kutatua tatizo
- mwanaume kuhama chumba naamini kulikuwa na tatizo kabla ya kuambiwa ujinga hivyo ndo kaona sehemu ya kumalizia hasira lakini hakufanya jambo sahihi
 

Ujinga siyo tusi ni fact. Nadhani kosa lake ni kuwa ali-jump kwenye conclusion kuwa mme wake ni mjinga. Angemuuliza kwanza kwanini ameamua kwenda bila mke baada ya kualikwa na huyo mjane.
 
huyu mjane nae bwana kwanini amualike mme bila mkewe ..
Kama sio kutafuta visa vya mama mwenye nyumba ..waambie wasameheane wagange yajayo hilo kosa sio la kufanya mme kuhama chumba ..
Na huyo mke wa jamaa nae kwa nn amuite mmewe mjinga wakati wanalala kitanda kimoja wanaume hawapendagi kudhalilishwa namna hiyo.
waambie wasikosane
 

hapo ndo inaonyesha kuna tatizo kati ya mjane na mke wa jamaa
 
pana walakini, kwa nini mke hakualikwa? Hata kama ukaribu ukaribu usipitilize. Labda mume anagonga kweli huyo mjane. Na inawezekana mume ni mjinga kweli(maana ukiachilia hlo hujui mangapi afanyayo )kudhihrisha ujinga wake badala ya kuketi na mkewe wawekane wazi kahama chumba
 

hapa nadhani kuna zaidi ya hilo ila mwanaume kaona nitoke vipi katumia hiyo kama sababu ... sijajua kama kulikuwa na magomvi kabla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…