Kipenzi Chao
Member
- Oct 12, 2010
- 99
- 4
Ukiwa mwanaume, umeoa na umekuwa na mzunguko wa hapa na pale katika kutafuta mkate wa familia. Umebahtika kumpata mtoto wako mmoja....! Umekuwa ni wa dunia ya leo na hivyo ukawa mmepanga na mkeo kuweka interval fulani katika maamuzi ya kumtafutia mwana wenu mdogoye...! Lakini ukiwa safarini ukawa na tabia ya kuwasiliana na mkeo mara kwa mara, na katika mawasiliano hayo mkeo akakudokeza jambo lilikupelekea kuumia ilhali imekuwa vigumu kuamini; ya kuwa mama yako mzazi eti anamshauri mkeo abebe mimba without your concern....!!!
Uliporudi ulimuuliza mkeo vizuri kwa kuwa fikra za kwamba huenda mkeo anamsingizia mama yako jambo kama hilo, na akafafanua kwa undani. Nawe ukaamua kufanya uchunguzi wa kina, na hatimaye ukabaini ya kuwa ni kweli mama yako alipata kumshauri mkeo jambo kama hilo...!
SWALI:

- Ukiwa mwanaume utalishughulikiaje hilo swala?
- Ukiwa mke wa mtu, je, wewe ungechukua hatua ipi juu ya ushari wa mama mkwe?
- Ukiwa mzee, mwenye kulea ndoa ya wanao, ni nini hasa kinachowafanya wazee kuwa na tabia kama hii?