Jamani naomba kueleweshwa hivi kwa nini kusiwepo na kipindi cha ukomo cha ubunge kama ilivyo kwa raisi.
Raisi TZ ana vipindi viwili vya miaka mitano mitano cha kuwa raisi.
Unakuta mbunge huyohuyo anakuwa mbunge zaidi ya miaka 35 yaani sawa na vipindi 7 vya miaka mitano mitano, mpaka huyo mbunge anachoka ile mbaya na inafikia hatua hawezi tena kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jimbo lake.
Au kukiwepo na ukomo kwa ubunge tatizo tunaweza kujikuta tunapata uhaba wa mawaziri? Maana huwezi kuwa waziri bila kuwa mbunge kwanza.
Labda inawezekana bongo tuna uhaba wa watanzania ambao wanaweza kuwa wabunge.

Kulifuta? Ya akina Richmond yangeibukia wapi? Tulipunguze Bunge letu. Ni kubwa mno kwa uchumi wetu wa sasa. Kila Halmashauri/ Manispaa iwe na Mbunge mmoja tu makini. Serikali yetu isiundwe na Wabunge. Baraza la Mawaziri liwe dogo na wizara ziwepo KIKATIBA sio Rais aachiwe kuunda wizara kulingana na idadi ya washikaji/wapambe/wafadhili alionao.The real question is, kwa nini bunge lisifutwe kabisa?
Mi sioni kazi yake.
Kulifuta? Ya akina Richmond yangeibukia wapi? Tulipunguze Bunge letu. Ni kubwa mno kwa uchumi wetu wa sasa. Kila Halmashauri/ Manispaa iwe na Mbunge mmoja tu makini. Serikali yetu isiundwe na Wabunge. Baraza la Mawaziri liwe dogo na wizara ziwepo KIKATIBA sio Rais aachiwe kuunda wizara kulingana na idadi ya washikaji/wapambe/wafadhili alionao.
The real question is, kwa nini bunge lisifutwe kabisa?
Mi sioni kazi yake.
waziri mkuu pinda alitoa hoja juu ya kuwepo na ukomo kwa wabunge kuwa na ukomo maalum wa vipindi vitatu tu.. ila cha ajabu wadau wengi walimpinga,hasa wengi wao wakiwa ni wabunge wanaotetea matumbo yao hasa waliofanya majimbo kuwa mali zao binafsi. binafsi hoja ya kuwepo na ukomo ktk ubunge na pia ktk nyadhifa za kisiasa nakubaliana nalo kwa kzaidi ya 100%..kwa sasa nikiangalia utendaji kazi na ufanisi wa bunge naona ni kama mchezo wa kuigiza na pia mnaona ni kama sehemu ya kuchuma utajiri kwani hamna wanachokifanya, naamini kwa kuruhusu damu changa itasaidia kuleta hamasa na changamoto nyingi bungeni..nyie wadau wengine mnalionaje hili?