Je kweli hii ni nimonia?

vee5

Member
Joined
Oct 23, 2018
Posts
10
Reaction score
5
Wakuu habari za jioni naomba niwashilikishe tatizo langu na mwenye uelewa anaweza nipa ushauri.

Miez kama sita nyuma nilipatwa na kauvimbe sehemu yachini ya shingo yani kwenye shina la shingo.upande wakushoto

Kunasiku nilihisi kichomi kwenye moyo na nyuma ya bega pia nilihisi kichomi.
Nikaamua kwenda hosptal. Baada ya kumuona doctar nakumueleza akasema nichek x-rey.
Baadae majibu yakaja nina nimonia nikaandikiea sindano pamoja na dawa nikawa nimetumia. Na ule uvimbe nilipo muuliza dictor akasema nitezi yani (tonses)kwahiyo nikimaliza dawa utakwisha.

Lakini adi sasa bado iyohali ya huo uvimbe ipo jamani aliyewai kupitia hili tatizo naombeni maoni yenu moyo pia ulionyesha kwenye picha upo sawa .

Au anaejua dawa anielekeze huu uvimbe hauumi ila nahuhisi najiona nikotofauti .ukilinganisha naupande mwingine.

Mwakaa mmoja nyuma nilipitia kipindi kigumu cha msongo mkubwa wamawazo
Nasasa ndonaona hii hali awali aikuwa kunitokea. Nawasilisha wakuu unaweza ata nipaushauri hosptal gn niende naishi dar.

Lakini pia napochelewa kula nahisi tumbo kama linachomwa chomwa.nikila hali inapotea ila uvimbe bado upo.

Je vidonda vyatumbo vinaweza kuja na iyo effect ya uvimbe? na vichomi nyuma ya bega.?
 
Nenda kamuone Daktari wa KIFUA KIKUU NA UKOMA atakusaidia shida yako
 
Uvimbe wako unaweza usiwe na uhusiano na dalili unazoelezea. Cha muhimu: hapa utapata majibu ya kubuni tu ambayo yatakuchanga zaidi. Nenda hospital kama Muhimbili, Aghakhan au TMJ umwone daktari. Kulingana na anavyokuona atakuandikia vipimo kabla ya kukutibu kama una tatizo. Hlafu kuhusu tumbo siku ukienda mwombe dr upime kama una bacteria wanaoitwa H. Plylori kwani ni common sana Tanzania na ndiyo wanaosababisha vidonda vya tumbo kwa sehemu kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…