Je kwenye unga wa lishe naweza ongeza dagaa na ndizi?

Je kwenye unga wa lishe naweza ongeza dagaa na ndizi?

Digaller

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2009
Posts
798
Reaction score
541
Habarini humu,

Nimejaribu kutafuta kama kuna jukwaa la afya ila nimekosa/sijaliona so nikaona si vibaya kwakua humu kuna doctors basi mnaweza kunipa ushauri mzuri zaidi kuhusu lishe, ndio namaanisha ''unga wa lishe kwa mtoto au hata mtu mzima.

Je kuna ubaya/faida gani kwa kuongeza unga wa lishe kwa kuweka dagaa/samaki na ndizi kwa kusaga pamoja kwaajili ya afya ya mtoto?

Namaanisha kwa mseto huu, mahindi+soya+karanga+ulezi+ndizi+dagaa/samaki je kuna faida kwa mtoto kuliko liishe asili ''ambayo tumeizoea'' i mean unga wa ulezi.

Na je kuna madhara yeyote kwa kuanza kumpa mtoto mdogo mlo huo hapo niliotaja hapo juu?

Na je ipi ni faida kiafya ambayo mtoto atapata kwa kula mlo tajwa hapo juu?

Natanguliza shukrani zangu kwenu doctors, pia naomba wale doctors wa afya ya mama na mtoto ndio mngenifafanulia zaidi kuhusu huu mlo ili nijue kama naweza pata faida zaidi ya kumpa mtoto cerelaki.
 
unga wa lishe ni mchanganyiko wa kila kitu siku hizi, kuanzia unga wa muhogo, mahindi, mchele, uwele, mtana, korosho, ngano ,ufuta, maharage, dagaa, kama unakisha broilers achana na haya makitu!
 
Inawezekana kuweka Dagaa lakini lazima kuandaliwa kwa kusagwa na kuwa unga. Anaweza kupewa mtoto wa kuanzia miezi 9 na kuendelea kwa sababu:- Uwiano wake wa hisia katika kinywa umeanza kuimarika kwamba hisia za chengachenga za nyama ya samaki haziwezi kumtapisha.
Mlo wake uwe na mchanganyiko ufuatao
1. UNGA WA MAHINDI + UNGA WA SOYA + UNGA WA DAGAA + UNGA WA KARANGA
AU
2. UNGA WA MAHINDI + UNGA WA SOYA + UNGA WA DAGAA + UNGA WA MBEGU ZA MABOGA
AU
3 UNGA WA MAHINDI + MAZIWA FRESH + UNGA WA DAGAA + UNGA WA MBEGU ZA UFUTA
HEBU TUANGALIE KAMA MLO HUU UNATUPA VITUTUBISHO KAMILI?
1. Wanga = unga wa mahindi
2. Protini = unga wa soya au maziwa fresh
3. Mafuta = mbegu za karanga, maboga na ufuta
4. Vitamini na madini = Unga wa samaki/ dagaa
Mlo wetu umekidhi vigezo vya kutengeneza mlo kamili
 
UNGA WA DAGAA UNA FAIDA ZIFUATANZO KWA MTOTO………
1. Unga wa Dagaa ni kinga ya moyo. Dagaa labda inajulikana kuwa samaki wa mafuta na kwa hivyo chanzo kizuri cha asidi ya mafuta ya omega-3, asidi muhimu ya mafuta ambayo mwili lazima upate kutoka kwa chakula kwani hauwezi kuifanya yenyewe.
Asidi ya mafuta ya Omega-3 kwa asili ni ya kuzuia uchochezi na kinga ya moyo kwani imegundulika kuwa na athari nzuri dhidi ya atherosclerosis, shinikizo la damu na thrombosis.
2. Unga wa Dagaa zinasaidia afya nzuri ya akili
Asidi ya mafuta ya Omega-3 pia imegunduliwa kusaidia afya njema ya akili kwa kuzuia hali kama vile wasiwasi na mfadhaiko na kusaidia kuongeza viboreshaji muhimu vya neurotransmitters (kemikali za ubongo) katika ubongo, pamoja na serotonin.
3. Husaidia kutengeneza seli nyekundu za damu
Vitamini B12 inayotoka kwenye dagaa ina jukumu muhimu katika utengenezaji wa seli nyekundu za damu, ambazo husaidia kusafirisha oksijeni kuzunguka mwili.⁠
4.mtoto anapokula unga wa dagaa hapati shida ya mmeng’enyo wa chakula kwa kuwa Unga wa Dagaa kwa ujumla wake wamejaa asidi muhimu za Amino ambayo husaidia mfumo wa chakula pamoja na ukuaji wa ubongo na mfumo wa neva za mtoto.
5. faida nyingine za Unga wa Dagaa kwa mtoto kuwa ni virutubisho vyake hushiriki kikamilifu katika utengenezaji wa homoni na michakato ya kimetaboliki ambayo yote hayo ni sehemu ya afya ya mtoto mwenye nguvu
6. Unga wa dagaa pia ni chanzo kizuri cha Vitamin B12, ikiwa ni chanzo kizuri cha pili baada ya maini. Vitamin hii hufanyakazi kubwa ya kuboresha ustawi wa moyo na hivyo kuwa chakula kizuri cha kumpa ahueni au kinga madhubuti mlaji dhidi ya magonjwa ya moyo.
7. Unga wa DAGAA NA MARADHI YA KANSA
Kwa miaka mingi, watafiti wameona jinsi ambavyo dagaa inavyoweza kudhibiti seli zinazosambaza saratani mwilini. Hivyo imethibitika pasi na shaka kuwa virutubisho vilivyomo kwenye dagaa huweza kutoa kinga kubwa dhidi ya ugonjwa wa saratani.
 
Back
Top Bottom