Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
NI NANI aliyevumbua Amerika?
Hakuna anayejua kwa hakika. Jibu lategemea sana jinsi unavyoelewa maneno “kuvumbua” na “Amerika.” Kwa vyovyote vile, nchi hiyo kubwa ilikaliwa na watu kwa mamia ya miaka kabla Wazungu hawajaijua. Christopher Columbus alirudi Ulaya mapema mwaka wa 1493, na kusimulia juu ya safari yake ya kwanza huko Amerika. Alikuwa amefika kwenye visiwa vya West Indies. Lakini hakuwa Mzungu wa kwanza kufika “ulimwengu [huo] mpya” wa ajabu. Yaelekea Waskandinavia wenye nywele za manjano walikuwa wamewasili bara la Amerika Kaskazini miaka 500 mapema.
Miaka elfu moja iliyopita, yamkini maji ya bahari ya Atlantiki Kaskazini yalikuwa baridi na yenye hali ya kubadilika-badilika kama yalivyo siku hizi. Baharia anaweza kufikiri kwamba anajua upepo na mikondo ya bahari, lakini ukungu na dhoruba zinaweza kufanya iwe vigumu kwake kujua alipo na anakoelekea kwa majuma kadhaa. Kulingana na hekaya moja ya kale ya Waskandinavia, jambo hilo ndilo lililompata baharia mjasiri mchanga, Bjarni Herjolfsson. Ijapokuwa alipotea baharini, huenda alipata bara jipya!
Jambo hilo lilitukia katika zama za Maharamia Waskandinavia wa kale, walipovuka bahari na kutawala sehemu nyingi za Ulaya. Merikebu zao nzuri nyembamba zilisafiri kutoka pwani ya Norway hadi pwani ya Afrika Kaskazini na kwenye mito ya Ulaya.
Kulingana na kitabu cha Saga of the Greenlanders (Hekaya ya Watu wa Greenland), Bjarni alisafiri hadi Norway na akakaa huko kwa muda mrefu. Majira ya baridi ya mwaka wa 986 B.K. yalipokuwa karibu kuanza, alirudi Iceland akiwa na bidhaa nyingi. Alishangaa alipojua kwamba baba yake alikuwa ameondoka Iceland katika msafara wa merikebu ulioongozwa na Erik the Red. Walihamia nchi kubwa ambayo Erik alikuwa amevumbua upande wa magharibi wa Iceland. Erik aliiita nchi hiyo Greenland. Mara moja Bjarni mchanga alifunga safari ya kwenda Greenland. Lakini upepo ukageuka. Mabaharia waliona ukungu tu. Hekaya inayotajwa juu inasema kwamba “kwa siku nyingi hawakujua walikoelekea.”
Mabaharia walipoona nchi kavu hatimaye, nchi hiyo haikulingana na ufafanuzi waliopewa wa Greenland. Pwani ilikuwa na mimea mingi, vilima, na misitu. Walisafiri kuelekea kaskazini huku pwani ikiwa upande wa kushoto. Walipoona nchi kavu tena, nchi hiyo pia haikulingana na ufafanuzi wa Greenland. Hata hivyo, baada ya siku kadhaa, mandhari ya nchi ilikuwa tofauti—yenye milima-milima na barafu. Kisha Bjarni na mabaharia wenzake wakageuka kuelekea mashariki wakiacha pwani na mwishowe wakafika Greenland na makao ya wale Waskandinavia waliosafiri katika msafara wa Erik the Red.
LEIF ERIKSSON AANZA SAFARI RASMI
Yaelekea wakati huo ndipo Wazungu walipoiona kwa mara ya kwanza bara lililokuja kuitwa Amerika Kaskazini. Yale ambayo Bjarni alikuwa ameyaona yaliwavutia sana Waskandinavia wenzake huko Greenland. Nchi yao yenye baridi ilikuwa na miti michache tu, kwa hiyo, ili kujenga na kurekebisha merikebu na nyumba walitumia mbao zilizopeperushwa pwani na upepo au mbao walizosafirisha kutoka ng’ambo, jambo ambalo liliwagharimu fedha nyingi. Lakini kumbe kulikuwako nchi yenye misitu na miti mingi sana upande wa pili wa bahari kuelekea magharibi!
Mwana mchanga wa Erik the Red, Leif Eriksson, alivutiwa na nchi hiyo mpya. Leif alifafanuliwa kuwa “mwanamume mkubwa, mwenye nguvu, mwenye sura nzuri na mwenye hekima.” Yapata mwaka wa 1000, Leif Eriksson alinunua merikebu ya Bjarni, naye pamoja na mabaharia wengine 35 wakaanza safari ya kutafuta pwani ambazo Bjarni alikuwa ameziona.
NCHI TATU MPYA
Ikiwa hekaya ni za kweli, Leif alifika kwanza kwenye nchi isiyo na nyasi iliyokuwa na barafu kwenye nyanda za juu. Nchi hiyo ilifanana na bamba la mwamba, kwa hiyo Leif aliiita nchi hiyo Helluland—maana yake, “Nchi ya Bamba la Mwamba.” Huenda wakati huo ndipo Wazungu walipoingia kwa mara ya kwanza katika bara la Amerika Kaskazini. Wanahistoria wa siku hizi wanaamini kwamba Helluland ilikuwa Kisiwa cha Baffin huko kaskazini-mashariki mwa Canada.
Waskandinavia hao wavumbuzi waliendelea na safari yao kuelekea kusini. Walipata nchi nyingine iliyokuwa tambarare na yenye misitu na pwani zenye mchanga mweupe. Leif aliiita nchi hiyo Markland, maana yake, “Nchi Yenye Misitu,” nayo hudhaniwa leo kuwa Labrador. Punde si punde, walivumbua nchi ya tatu yenye kuvutia hata zaidi.
Hekaya inasema hivi: “Walianza safari ya baharini na kusafiri kwa siku mbili, kukiwa na upepo wa kaskazini-mashariki kabla ya kuona nchi kavu.” Walipendezwa sana na nchi hiyo mpya hivi kwamba waliamua kujenga nyumba kadhaa na kukaa huko hadi mwisho wa majira ya baridi. Wakati wa majira ya baridi “halijoto haikushuka kamwe chini ya kiwango cha mgando na nyasi zilinyauka kidogo tu.” Baadaye, mmoja wa wanaume hao alipata hata zabibu na mizabibu; kwa hiyo Leif Eriksson akaita nchi hiyo Vinland, yamkini jina hilo linamaanisha “Nchi ya Divai.” Baada ya majira ya baridi wanaume hao walirudi Greenland, merikebu zao zikiwa zimejaa mazao ya Vinland.
Wasomi wa siku hizi wangependa sana kujua mahali ilipokuwa nchi hiyo ya Vinland yenye nyanda za malisho na zabibu, lakini hadi leo hawajajua. Baadhi ya watafiti wanaonelea kwamba ufafanuzi katika hekaya za kale unalingana na mandhari ya nchi ya Newfoundland. Eneo moja la makao lililofukuliwa huko Newfoundland linathibitisha kwamba Waskandinavia walifika kwenye kisiwa hicho. Hata hivyo, wanasayansi wengine wanadhani kwamba Vinland ilikuwa kusini zaidi na kwamba eneo hilo huko Newfoundland lilikuwa tu kituo cha kusafiri kwenda Vinland.*
KUNA UTHIBITISHO GANI?
Hakuna anayeweza kupatanisha habari za hekaya hiyo ya Waskandinavia wa kale na nchi za siku hizi. Maelezo machache yasiyoeleweka wazi ya hekaya hizo yamewatatanisha wanahistoria kwa muda mrefu. Hata hivyo, eneo lililofukuliwa huko Newfoundland katika miaka ya 1960 na 1970 karibu na kijiji cha L’Anse aux Meadows linaonyesha wazi kwamba Waskandinavia walifika Amerika kabla ya Columbus kuwasili huko. Hapo kuna magofu ya nyumba ambazo bila shaka zilijengwa na Waskandinavia na vilevile tanuri la chuma na vitu vingine ambavyo vinakadiriwa kuwa vya siku za Leif Eriksson. Hivi majuzi Mvumbuzi Mdenmark anayefanya kazi huko kusini mwa Newfoundland alivumbua jiwe lililokuwa limechongwa kwa ustadi, ambalo yamkini lilitumiwa kusawazisha merikebu fulani ya Maharamia.
Safari za Waskandinavia wa kale za kwenda nchi mpya mbalimbali huko magharibi hazikufichwa. Leif Eriksson alisafiri hadi Norway ili kuripoti kwa mfalme wa Norway yale aliyokuwa ameona. Adam wa Bremen, Mjerumani aliyekuwa mwanahistoria na mkuu wa shule fulani ya kanisa, alisafiri hadi Denmark yapata mwaka wa 1070 ili kujifunza juu ya nchi za kaskazini. Mfalme Sweyn wa Denmark alimweleza juu ya Vinland, ambako mizabibu inayotokeza divai bora hukua. Mapokeo hayo yakawa sehemu ya simulizi la Adam wa Bremen. Kwa hiyo, wasomi wengi huko Ulaya walijua juu ya nchi za magharibi ambazo Waskandinavia walikuwa wametembelea. Isitoshe, masimulizi ya kale ya kihistoria ya Iceland ya karne ya 12 na 14 yanataja safari za baadaye za Waskandinavia za kwenda Markland na Vinland zilizokuwa magharibi ya Greenland.
Yamkini Christopher Columbus pia alijua juu ya safari hizo za kwenda Vinland zilizofanywa miaka 500 kabla ya siku zake. Kulingana na kitabu kimoja juu ya Vinland, huenda Columbus alisafiri hadi Iceland ili kuchunguza maandishi yaliyopatikana huko kabla ya kuanza safari yake maarufu ya mwaka 1492 na 1493.
WASKANDINAVIA WA KALE WALIPATWA NA NINI?
Hakuna rekodi inayoonyesha kwamba Waskandinavia wa kale waliishi Amerika daima. Huenda walijaribu kuishi huko; lakini hawakufaulu kwa sababu hali ilikuwa ngumu na walishindwa vitani na wenyeji wa Amerika—ambao Maharamia waliwaita Skraeling. Wazawa wa Erik the Red na wa mwana wake Leif Eriksson walikabili hali ngumu huko Greenland. Hali ya hewa ilizidi kuwa mbaya, na chakula na vitu vingine vya lazima vikawa haba. Yaelekea Waskandinavia walitoweka kabisa huko Greenland baada ya miaka 400 au 500. Habari ya mwisho iliyoandikwa juu ya Waskandinavia huko Greenland inahusu arusi iliyofanywa katika kanisa moja la Greenland mwaka wa 1408. Baada ya zaidi ya miaka 100, Wajerumani waliosafiri kwa merikebu ya biashara walipata makao ya Waskandinavia yasiyokuwa na wakazi. Walipata tu maiti ya mwanamume mmoja, aliyekuwa na kisu chake bado. Baada ya hapo hakuna habari yoyote inayotaja Waskandinavia huko Greenland hadi karne ya 18 wakati ambapo watu wa Norway na Wadenishi walihamia huko.
Hata hivyo, huko Greenland ndiko manahodha wajasiri Waskandinavia walikoanza safari zao za kwenda ulimwengu mpya. Mtu anaweza kuwazia wale mabaharia wajasiri wakivuka bahari ambayo hawakuwa wameizoea, kwa merikebu zao zenye matanga ya mraba hadi wanapoona na kustaajabia pwani mpya. Hawakufikiri kamwe kwamba miaka 500 baadaye, Christopher Columbus angesifiwa kuwa mvumbuzi wa Ulimwengu huo Mpya.
NB;Waskandinavia ni wale watu wanaotokea katika nchi za Norway,Sweden na Finland