Je, lifti ikizidiwa uzito inafunga mlango?

Je, lifti ikizidiwa uzito inafunga mlango?

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Wajuzi wa mambo naomba kupata ufahamu kidogo, kutokana na suala la lifti kuporomoka Millennium Towers nimeona baadhi ya wadau wakisema lift ikizidisha uzito haifungi wengine wakidai inatoa maelekezo kuwa watu wamezidi na kuwataka kupungua.

Je, ni kweli wanaodai hivyo wako sawa? Na kama wako sawa sababu iliyotajwa ya kuporokwa kwa kuzidisha uzito si sababu sahihi kwa hiyo kuna sababu ambayo haijatajwa? Kamba ndivyo aliyetoa sababu amekurupuka au kuna jambo linafichwa ili kusiwepo kuwajibika kutokana na jambo hilo?

Wajuzi na wataalamu na wenye uzoefu na matumizi ya lifti naomba mtufungue macho ili watu waweze kupata uwanja wa kuhoni zaidi juu ya jambo hili.

1684929776514.png

Pia soma: Lift ya Jengo la Millennium Towers yaanguka ikiwa na watu, kuzidisha idadi ya Watu yatajwa kuwa chanzo
 
Zinafunga vizuri tu. Kuna hii ya jengo flani hivi Ikifail inarudi kimyakimya vuuuuuu mpaka basement na kujizima huko Sasa mpaka mje mtolewe 😂😂😂😂

Nadhani pia ni za kichina zile grade ya bei chee, zinamuonekano mzuri ila ufanisi hakuna.

Mnaweza kuwa watu watatu na bado ikafail na sio mbovu mnaambiwa tu kilo zilizidi.
 
Lifti zote za mjapani zikizidi uzito hujizima automatiki na za mchina zikizidiwa zinapiga alamu.
 
Wajuzi wa mambo naomba kupata ufahamu kidogo, kutokana na suala la lifti kuporomoka Millennium Towers nimeona baadhi ya wadau wakisema lift ikizidisha uzito haifungi wengine wakidai inatoa maelekezo kuwa watu wamezidi na kuwataka kupungua.

Je, ni kweli wanaodai hivyo wako sawa? Na kama wako sawa sababu iliyotajwa ya kuporokwa kwa kuzidisha uzito si sababu sahihi kwa hiyo kuna sababu ambayo haijatajwa? Kamba ndivyo aliyetoa sababu amekurupuka au kuna jambo linafichwa ili kusiwepo kuwajibika kutokana na jambo hilo?

Wajuzi na wataalamu na wenye uzoefu na matumizi ya lifti naomba mtufungue macho ili watu waweze kupata uwanja wa kuhoni zaidi juu ya jambo hili.

Pia soma: Lift ya Jengo la Millennium Towers yaanguka ikiwa na watu, kuzidisha idadi ya Watu yatajwa kuwa chanzo
Kwa kawaida, uzito ni sehemu ya interlocking mechanism au condition ya lift kuendelea kufanya kazi. Kwamba ifunge mlango then ipande juu au ishuke chini kutegemeana na ilikoamriwa kwenda. Kama uzito ukizizidi, haifungi mlango na kuna kimlio kinasikika kuashiria uzito umezidi, au nyingine kuna programed machine inaongea kwamba kuna overweight kama inavyosema floor uliyopo. Sema kwenye matengenezo, inawezekana kabisa kulifanyika bypass na conditions nyingine kuondolewa.
 
Uchunguzi wa kina ufanyike maana sasa hivi nchi yetu ina magorofa mengi sana yanayotumia lift,ikiwezekana hata kuwe kuna mamlaka itakayowekwa kukagua lift nchi nzima...
 
Back
Top Bottom