SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,240
- 4,265
Huwa nasikiliza sana vipindi vya mapishi kwenye tv na redio. Kinachonishangaza ni wingi wa matumizi ya maneno ya kumiliki (possessives) eg yangu, yako yetu etc . Mathlani mpishi atasema hivi kuhusu namna ya kuandaa samaki:Unamchukua samaki wako unampaa vizuri kisha unamwanika mpaka akauke. Akikauka chukua mafuta yako uyaweke kwenye kikaangio chako. kisha weka jikoni.................
Kwa mawazo yangu nilifikiri haya maelekezo yangekuwa bora zaidi kama hayo maneno niliyobold yangeondolewa.
Mwasemaje wataalamu wa kiswahili?
Kwa mawazo yangu nilifikiri haya maelekezo yangekuwa bora zaidi kama hayo maneno niliyobold yangeondolewa.
Mwasemaje wataalamu wa kiswahili?