Natumia Apple Macbook Pro M1 chip 8GB RAM / 512GB SSD
In my experience, naweza kufungua Jetbrains IDE mbili i.e Android Studio/Intelli J na PHPStorm kwa wakati mmoja.
Nkafungua Android emulator na iOS Simulator kwa wakati mmoja.
Na bado nkafungua Google chrome ikiwa na tabs kama 10 hivi, na baadhi yake zikiwa zina stream Video.
Jetbrains IDE ni nzuri sana kwenye programming ila ziko very expensive/hungry on resource. On average hizi tools zote nilizo simulate hapo juu zinaweza tumia 8GB RAM yote, ila sijawai kuona lagging, fan kuunguruma au PC kuchemka hata siku moja.
Nimejaribu ku simulate kuwa ukiwa mwanafunzi wa C/S kuna moment utajikuta katika scenario ambako una code Frontend/Mobile application kwa Flutter(utaitaji kutumia Android studio, android emulator, iOS simulator) na wakati huo huo frontend yako ikawa ina communicate na backend yako iliyoandikwa e.g kwa PHP hivo kukuitaji kufungua IDE nyingine na wakati huo huo ukawa unaitaji kufungua Browser/G.Chrome ku browse resources/documentations mtandaoni.
Katika scenario hiyo ndo utaona M1 Chip pc zilivo moto wa kuotea mbali.
Mm nimetumia PC za windows tena high end, nkatumia PC za apple Intel Chipset, naweza kukupa testimony kuwa sijawai kuona perfomance na experience iliyoweza kuifikia computer ya M1 chip.
Hivo nakushauri chukua M1 chip computer, tena ukiweza upgrade kidogo uende Macbook pro, you will never regret and mind you, hauwezi pata PC inakaa charge takribani masaa 24 nje na hizo nilizotaja au superiors zake.
Kazi kwako.