Je, mahakama ya mwanzo ina mamlaka kushughulikia kesi iliyo nje ya wilaya au mkoa?

Mwilabheghe

Member
Joined
Feb 14, 2018
Posts
30
Reaction score
14
Kwenu mawakili wasomi.
Naomba kujua mipaka ya mahakama za mwanzo kisheria. He inaweza kuendesha kesi ambayo mshitakiwa anaishi wilaya nyingine?

Mfano, uliwahi kuishi Kilolo Iringa kuna mtu ulikuwa unamdai akahama anaishi Makete Njombe. Mtu akachukua summons mahakama ya mwanzo "x" Kilolo na kumfuata Makete.

Je, ni sawa? Kama si sawa afanyeje, huyu respondent? Akigoma kusaini atakuwa amedharau mahakama?
 
Mkuu Mwilabheghe Mahakama ya mwanzo inayo mamlaka ya kumwita shaurini mtu aliyeko nje ya mamlaka yake (wilaya au tarafa/kata) pale tu anahitaji kujibu mashtaka au kutoa ushahidi juu ya kesi iliyotokea ndani ya eneo lililo chini ya mamlaka yake.

Kwa hiyo basi kama mdai wako aliishi wilayani kilolo wakati madai yalipoanza, mahakama ya mwanzo inayo mamlaka ya kumwita hata kama yuko makete, na kisheria anatakiwa kutii wito.
 
Nashukuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…