Je, mahali panapoitwa Ngende ni pakusadikika?

Ngende
Apo mkwele hakuna ngende,, ila kuna sehemu panaitwa bwawani, apo napo watu huenda kwa ajili ya kufanya maombi na ibada mbalimbali,, kuna bwawa ambalo wenyewe huamin kwamba kama unashida unaenda apo unafanya maombi unaoga ktk hilo bwawa kisha shda zako huisha,, ngende iko liwale,, kutoka apa nilipo , nyangao mpaka bwawani ni jero tuh nauli,,
 
Sio kweli..maelezo ya sigara kali ndio yako sahihi..hii yako chai.
 
vp Alitii maagizo?
 
Nilifika huko mwaka 2016,baada ya kupata msukosuko kazini,binafsi nikili tu kuwa sikuona jipya kama ambavyo ilikuwa ikisimuliwa,zaidi ni uhuni na utapeli uliokithiri kwa watoa huduma,kila kona unambwa pesa kama uko kituo cha ombaomba,mbaya zaidi baada ya kupata nafasi ya kuonana na bibi mwrnyewe ambaye anaitwa BIBI JUMWITE ambayehajui kiswahili ila KINGINDO PEKEE, Kuna mtafasiri wake ambaye usipo kuwa makini unaweza maliza hata milioni,baada ya hapo unakazimishwa kuweka nadhiri ya kiasi cha pesa ambacho utakipeleka baada ya kufanikiwa shida yako.Hawa jamaa wapo Liwale mkoa wa lindi eneo linaitwa MPIGA MITI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahani Mkuu,mimi najua ngende iko liwale kijiji cha mpiga miti huko nangao tens duh!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa, ni wahuni tu walinikera sana nilifika huko mwaka 2006
 
Huko kibali Cha ukaazi Ni grease bila Shaka

Sent using Jamii Forums mobile app
Huko ni balaa. Uki default masharti, jina litahusika.
Tukiacha utani, mengi yameandikwa humu ni chai na matango pori.
Ni sehemu ya kawaida sikuona kitu cha ajabu hata.
Tulikuwa Liwale kikazi. Out of curiosity tukaenda watu wanne. Walitupokea vizuri na tulipiga nao stori. Mwisho tukaulizwa shida yetu. Tukasema tulitaka kupajua tu. Wakasema mwenye shida ya utajiri, cheo kazini au zindiko la nyumba au biashara, atasaidiwa. Tuliwapoza kidogo tukaondoka.
 
Kunchelile maalongo?
 
Hapo MTAFITI ukawa amemaliza UTAFITI!!!!!!!!!!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Ngende ipo mkoa wa Lindi wilaya ya liwale tarafa ya nanjilinji kata ya mpigamiti, haya maelezo yako futa usije ukamtoa ndg yetu kwenye kusudio lake, maana umetaja hapa karibu tu nyangao, ngende ni mbali huna uwezo wa kutoka leo dar ukafika lkn hapo mkwela ukipita mtama unaingia mkwela.
Wasalam

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…