Je! Mahari ni suala la kisheria?

pambe samanini

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2015
Posts
368
Reaction score
169
Nataka kufahamu zaidi kuhusu utoaji wa mahari kwenye masuala ya ndoa kama:-
1. Mahari ni nini?
2. Mahari ni muhimu katika ndoa?
3. Bila mahari ndoa hiyo ni batili?
4. Nani anahusika kupokea na kutoa mahari?
5. Je,! Wasiotoa mahari wanatenda kosa gani kisheria?
Karibuni ndugu kwa msaada wenu
 
Kwa Kanisa katoliki, kama hujatoa mahari huoi.
 
Ndio bila mahari, ndoa ni ubatili. Tena sana, ila ni kwa upande wa Imani zaidi hasahasa ya Kikristu.
 
Zamani katika makabila ya kanda ya ziwa, aliyekufa mhusika mkuu wa kutoa mahari alikuwa mzazi wa kiume, na hata sasa ni hivyo, ila kama mzazi wa kiume ni maskini au hayupo, basi anayehusika kutoa mahari ni wewe.
 
Kwa sheria za Kitanzania, hatendi kosa lolote ila kwa sheria za Kanisa katoliki ni kosa kubwa kubwa la kukupeleka Kuzimu.
 
Mahari ni makubaliano kwa vile ni sharti la ndoa ...Usipende kuruka stage si mila wala dini mahari ni muhimu sema kiwango sio constant .

Sidhani kama unataka kuoa na majukumu ya ndoa mtoto wa kiume ushindwe mahari .
 
We subiri ufumaniwe uozeshwe ndoa ya mkeka
 
Mleta mada bado hazikutoshi! Nakuuliza: Umezaa? Fikiria inafika jioni/usiku au siku kadhaa umuoni mtoto wako!! Patakalika? Bora awe amefariki ulie na kujua kila mtu atapitia njia hiyo na mwisho wa siku unatulia na maisha yanaendelea! Mtu au mtoto ameunganishwa na familia au ukoo alikozaliwa! Unapomchukua bila kibali cha familia au ukoo (kwa kushupaza shingo) ujue unajiingiza katika matatizo makubwa na ujue hayatakuacha/hayatawaacha salama mpaka mrekebishe na wazazi/familia yao! Hata kama mnajiona mko sawa na mahusiano yenu ya wizi, ni suala la muda tu (mtajikaza huku mmenigwa na tai shingoni). Binti wa watu kamwe usimchukue bila kibali cha wazazi! Fanya ufanyaro hata kwa kuwaomba na kuwaahidi kwa saundi kuliko kujifanya mwamba!
 
Mleta mada bado hajajibiwa swali lake kiufanisi!!
Kutoa mahari sio suala la kisheria! Unakuwa hujatenda kosa kwasababu huyo uliyemchukua kuwa mkeo naye anaakili angeweza kukataa! Kitendo cha kukubali kuondoka kwa wazazi wake na kuja kuanza kuishi na wewe wakati ana akili timamu (na ana umri wa miaka inayokubalika, mfano 18) kunakufanya muoaji hasiwe na kosa! Suala ni upande wa wazazi watalichukuliaje? wanaona mmewaletea dharau na ukikuta wazazi watata wanaweza kuja na kumchukua binti yao kwa nguvu na wewe mwanaume wakakulia njama na kukupa kibondo kikali hata kukuua! Kuna familia hazitaki kabisa kuunganishwa na koo/kabila/familia ya aina fulani kupitia kuoana! Nakupa mfano katika Biblia! (Mwanzo 34: nakuendelea). Mfano dhahiri hapa bongo nenda kamrubuni binti wa kihindi muweke ndani uone moto wake!
 
Ni kununua mwanamke kama nyanya
Hapana ni utaratibu wa kutambua malezi na makuzi ya huyo binti kwa wazazi wake na vile vile kuhakikishia wazazi wake na jamii kuwa unauwezo wa kumtunza na kujenga familia
 
Mbona kama hujamuelewa mtoa mada hivi,unamjibu kanakwamba kapinga maswala ya mahali.Yeye kauliza maswali na wewe mjibu kwa hoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…