Namshakende
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 671
- 1,644
Kila ninapokumbuka mahojiano(interview) yangu ya kwanza,nacheka sana. Ilikuwa kama filamu ya vichekesho, iliyojaa matukio ambayo sikutegemea kukutana nayo.
Siku hiyo, rafiki yangu aliniambia, "Kuna mchongo wa kazi kampuni X. Ngoja nikupatie." Bila kusita, nilianza safari yangu kutoka Kibada hadi Kigamboni, nikipanda vyombo vya usafiri vyote vilivyopo hadi Kimara. Nilifika kwenye kampuni, nikiwa nimevaa nguo zangu za kawaida za mtaani, nikiamini kuwa naenda kukabidhi vyeti vyangubtu! “si Mshikaji kanipati Mchongo”
Lakini nilipoingia kwenye chumba kimoja, nilipigwa na butwaa. Kulikuwa na jopo la watu wengi, wote wakiniangalia kwa macho makali. Nilikuwa nimevaa jeans, T-shirt ya Yanga, na sendo za kimasai. Nikajisemea Mshikaji kaniuzia Mbuzi kwenye gunia.Ili baki kidogo tu nitoroke kwenye kile chumba.
Mzee mmoja aliniuliza, "Je, wewe ni mwendesha bodaboda?" Nilijaribu kujizuia kucheka, lakini harufu ya jasho langu labda ilikuwa imenisaliti. Nilijua kuwa mavazi yangu na harufu yangu vilikuwa vimenipa picha mbaya kabisa.
Mahojiano yaliendelea, na maswali yalikuwa magumu sana. Rafiki yangu ambaye aliniambia kuhusu kazi hii, alikuwa anauliza maswali ya ajabu zaidi ya watu wengine! Nilikuwa nimechanganyikiwa kabisa.
Licha ya yote hayo, kwa bahati nzuri, nilipata kazi hiyo. Na hadi leo hii, kila ninapokumbuka mahojiano hayo, najifunza mambo mapya;
Nilijifunza umuhimu wa kujitayarisha vizuri kwa kila event , kuvaa nguo zinazofaa, na kuwa mtulivu hata katika hali ngumu.
Na muhimu zaidi, nilijifunza kwamba hata katika hali za aibu, kunaweza kuwa na matokeo mazuri. Na ndiyo maana hadi leo hii, ninaishukuru kazi hiyo, kwani ilinifungulia milango mingi katika maisha yangu.
Tuambie na wewe mahojiano yako ya kwanza yalikuwaje?