Je, mahojiano( interview) yako ya kwanza ilikuwaje?

Namshakende

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
671
Reaction score
1,644
Kila ninapokumbuka mahojiano(interview) yangu ya kwanza,nacheka sana. Ilikuwa kama filamu ya vichekesho, iliyojaa matukio ambayo sikutegemea kukutana nayo.

Siku hiyo, rafiki yangu aliniambia, "Kuna mchongo wa kazi kampuni X. Ngoja nikupatie." Bila kusita, nilianza safari yangu kutoka Kibada hadi Kigamboni, nikipanda vyombo vya usafiri vyote vilivyopo hadi Kimara. Nilifika kwenye kampuni, nikiwa nimevaa nguo zangu za kawaida za mtaani, nikiamini kuwa naenda kukabidhi vyeti vyangubtu! β€œsi Mshikaji kanipati Mchongo”

Lakini nilipoingia kwenye chumba kimoja, nilipigwa na butwaa. Kulikuwa na jopo la watu wengi, wote wakiniangalia kwa macho makali. Nilikuwa nimevaa jeans, T-shirt ya Yanga, na sendo za kimasai. Nikajisemea Mshikaji kaniuzia Mbuzi kwenye gunia.Ili baki kidogo tu nitoroke kwenye kile chumba.

Mzee mmoja aliniuliza, "Je, wewe ni mwendesha bodaboda?" Nilijaribu kujizuia kucheka, lakini harufu ya jasho langu labda ilikuwa imenisaliti. Nilijua kuwa mavazi yangu na harufu yangu vilikuwa vimenipa picha mbaya kabisa.

Mahojiano yaliendelea, na maswali yalikuwa magumu sana. Rafiki yangu ambaye aliniambia kuhusu kazi hii, alikuwa anauliza maswali ya ajabu zaidi ya watu wengine! Nilikuwa nimechanganyikiwa kabisa.

Licha ya yote hayo, kwa bahati nzuri, nilipata kazi hiyo. Na hadi leo hii, kila ninapokumbuka mahojiano hayo, najifunza mambo mapya;

Nilijifunza umuhimu wa kujitayarisha vizuri kwa kila event , kuvaa nguo zinazofaa, na kuwa mtulivu hata katika hali ngumu.


Na muhimu zaidi, nilijifunza kwamba hata katika hali za aibu, kunaweza kuwa na matokeo mazuri. Na ndiyo maana hadi leo hii, ninaishukuru kazi hiyo, kwani ilinifungulia milango mingi katika maisha yangu.


Tuambie na wewe mahojiano yako ya kwanza yalikuwaje?
 
Nilipigiwa simu saa nne usiku kuhusu mchongo x

Je nipo tyr nikaitikia ndiyo ?

Akaniambia andaa documents zote, kesho saa mbili Kuna mtu utakutana nae mwenge!

Usivae vikaptula vyenu hivyo! Nikamjibu ok....

Alini draftia barua ni Mimi kuitoa tuu, sasa umeme umekata ......

Bahati nzuri nguo zangu huwa zinakaa nadhifu always!

Kesho yake nikapokelewa na mwenyeji kuelekea ofisini

Nimekaa kuanzia saa tatu mpaka saa kumi huko ndo boss anakuja


Interview ikafanyika kwenye gari hata doc hakuziangalia ....... kikubwa nijifunze na nipige kazi.....

Ikaisha hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…