Je, mahusiano ya rafiki wa mpenzi wako yanaweza haribu mahusiano yako?

Je, mahusiano ya rafiki wa mpenzi wako yanaweza haribu mahusiano yako?

maxeric

New Member
Joined
Jul 31, 2024
Posts
4
Reaction score
7
Ningependa kufahamu, je mahusiano ya rafiki wa mpenzi wako ni jinsi gani yanayoweza athiri mapenzi yako?

Maana imekuwa ni changamoto sana, asilimia kubwa ya maisha ya mpenzi wangu yuko na rafiki yake kila sehemu. Sasa mapenzi ya rafiki yake ni yako moto hata mimi naona kbsa kweli yameiva, jamaa anamnunulia vitu, kupostiana kumepamba moto, anampeleka huku na huko hadi kuna mara kadhaa hadi na mpenzi wangu alikua akienda nao.

Sasa mimi nasoma MD nakuwa busy hata sina muda ki hivyo na hata pesa yangu hazijitoshelezi kufanya hayo yote, lkn sasa hivi karibuni mpenzi wangu amekuwa akizidisha story za mapenzi ya rafiki yake na mimi nakuwa nachangia lkn hii kitu inaniuma na ninahofia kuwa nitampoteza maana nahisi anatamani na mm nifanye kama anavyofanyiwa rafiki yake lkn sina uwezo na muda ki hivyo. Au ni woga wangu tu!

Swali langu ndio linakuja hapo, nataka tu kufahamu ni kwa njia zipi mapenzi ya rafiki wa mpenzi wangu wanaweza athiri mapenzi yetu na nichukue hatua gani?
 
Usichukue hatua yoyote
Muhimu huyo mpenzi wako ajue uhalisia wa maisha yako,ajue uko busy na chuo kwa hiyo huna muda wa kuwa nae mara nyingi

Kama ni wako atabaki na wewe
 
Back
Top Bottom